Tanzania kufungua rasmi ofisi za Ubalozi Indonesia

JAKARTA-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewasili Jakarta nchini Indonesia kwa ajili ya ziara ya kikazi, ikiwa ni pamoja na kufungua rasmi Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo hapo tarehe 22 Juni, 2023.
Mhe. Dkt. Tax baada ya kuwasili Jakarta amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Tembele katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta (CGK).



Akiwa nchini Indonesia Mhe. Dkt. Tax anatarajia pia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Mhe. Retno Marsudi, na kutembelea Chuo cha Diplomasia cha Indonesia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news