Tanzania yaahidi ushirikiano zaidi kwa wadau wa maendeleo

NA JOSEPH MAHUMI-WFM

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuhakikisha Tanzania inatimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 (SDGs), ambayo pamoja na mambo mengine, yamelenga kuondoa umasikini katika jamii.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Jenifa Omolo (wa tano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN), baada ya warsha kwa ajili ya kujadili na kuthibitisha taarifa ya mapitio ya hiari ya nchi ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs), iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati akifungua warsha ya wadau kwa ajili ya kuthibitisha taarifa ya mapitio ya hiari ya nchi ya utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, kabla ya kuwasilishwa katika Jukwaa la Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani Mwezi Julai, 2023.

Serikali imewasilisha taarifa ya mapitio ya hiari ya nchi ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu 2030 kwa wadau kuijadili na kuipitisha kabla ya, huku wadau hao wakiipongeza Serikali kwa uwazi na kupiga hatua kubwa ya utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu 2030.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Jenifa Christian Omolo, akifungua warsha ya wadau kwa ajili ya kujadili na kuthibitisha taarifa ya mapitio ya hiari ya nchi ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs), iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.

“Mchakato wa kufanya mapitio ya utekelezaji wa SDGs umekuwa shirikishi, na wa uwazi, ukishirikisha wadau wote muhimu nchini wakiwemo: Serikali Kuu; Sekta Binafsi; Asasi za Kiraia; Bunge; Mamlaka za Serikali za Mitaa; na Utafiti, pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu,” aliongeza Bi. Omolo.

Bi. Omolo alisema kuwa Tanzania, ilichagua kutekeleza ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu kwa kuyaasili katika mipango na mikakati ya kitaifa na ya kisekta na wakati mchakato wa kupitishwa kwa SDGs unafanyika, Tanzania ilikuwa inaandaa mpango wake wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 – kwa upande wa Tanzania Bara, na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini 2016-2020 au MKUZA III, kwa upande wa Zanzibar.
Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa - Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Mursali Milanzi, akizungumza jambo wakati wa warsha ya wadau kwa ajili ya kujadili na kuthibitisha taarifa ya mapitio ya hiari ya nchi ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs), iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.

Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Mursali Milanzi, amelima kuwa malengo yaliyofanikiwa katika ajenda kwa kipindi cha miaka mitano yametokana na ushirikiano wa wadau katika upatikanaji na matumizi ya takwimu.

“Serikali imekusudia kuimarisha zaidi upatikanaji wa takwimu ili kusaidia kurahisisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030” alisema Dkt. Milanzi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Jenifa Omolo (wa nne kulia), katika picha ya pamoja na wadau kutoka mashirikia ya Umoja wa Mataifa (UN), baada ya kufungua warsha kwa ajili ya kujadili na kuthibitisha taarifa ya mapitio ya hiari ya nchi ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs), iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma. 

Tanzania na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa, Septemba 2015, zilipitisha ajenda ya 2030 ya kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambayo, pamoja na mambo mengine, iliainisha Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ambayo kwa kifupi yanajulikana kama SDGs.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news