Madaktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakimlaza mgonjwa kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa moyo. Upasuaji huo umefanyika hivi karibuni nchini Zambia ambapo wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa hospitali ya Moyo Zambia walifanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye chumba cha juu upande wa kushoto wa moyo (Myxoma). Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child's Heart -SACH) la nchini Israel ndilo lililoratibu ufanyikaji wa upasuaji huo.


Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia, Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child's Heart -SACH) la nchini Israel na Congenital Heart Academy kutoka nchini Italia wakiwa katika kikao cha kuangalia ni namna gani JKCI itakavyowajengea uwezo wataalamu wa hospitali hiyo ili waweze kutoa huduma za upasuaji wa moyo.
Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia, Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child's Heart -SACH) la nchini Israel na Congenital Heart Academy kutoka nchini Italia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kuangalia ni namna gani JKCI itakavyowajengea uwezo wataalamu wa hospitali hiyo ili waweze kutoa huduma za upasuaji wa moyo.