Tanzania yawashirikisha wafanyabiashara wa Austria fursa zilizopo nchini

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna.

Dkt. Tax ameshiriki kikao hicho pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ambapo kwa pamoja walielezea jinsi serikali ilivyoboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini.

Wamewaelezea Wafanyabiashara wa Austria juu ya faida zinazoweza kupatikana kupitia uwekezaji au ubia na Serikali ya Tanzania au mtu binafsi.
Kaimu Balozi na mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Umoja wa Mataifa Vienna, Bi.Elizabeth Rwitunga akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna.

Dkt. Tax amewahakikishia Wafanyabiashara hao kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na usalama na ni kituo muafaka kwao kuwekeza mitaji yao na kufanya biashara.

Tanzania ni nchi yenye amani na usalama, kiufupi Tanzania ni njema na kwa hivyo mna uhakika na usalama wa mitaji yenu na kufanya biashara,” alisema Mhe. Waziri.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme wakifuatilia mkutano kati ya Wizara na Jumuiya ya Wafanyabiashara Austria jijini Vienna uliofanyika tarehe 13 Juni, 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Bw. Gilead Teri akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna.

Akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw. Khamis Dunia alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefungua milango ya uwekezaji na kuwakaribisha wenye nia ya kuwekeza Zanzibar katika maeneo ya utalii na miundombinu waje nchini kuwekeza na kujionea vivutio.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) amesema Serikali imeunganisha mifumo ya taasisi za usajili na uwezeshaji biashara ili kutoa huduma bora kwa wawekezaji. Taasisi hizo zinajumuisha TIC, NIDA, TRA, BRELA, Uhamiaji na Idara ya Kazi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji Zanzibar Bw. Khamis Dunia akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni, 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni, 2023.
Mmoja wa wafanyabiashara wa nchini Austria akizungumza katika kikao kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wafanyabiashara wa Austria kilichofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni,2023 kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali nchini kwa wafanyabiashara hao.
Baadhi ya wafanyabiashara wa nchini Austria walioshiriki mkutano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wafanyabiashara wa Austria kilichofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni,2023 kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali nchini kwa wafanyabiashara hao.
Baadhi ya wafanyabiashara wa nchini Austria walioshiriki mkutano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wafanyabiashara wa Austria kilichofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni,2023 kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali nchini kwa wafanyabiashara hao.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale Ali waambie wafanyabiashara hao kuwa eneo la utalii lina utalii wa aina nyingi ambazo wawekezaji wanaweza kuja nchini na kutembelea maeneo hayo na kuwekeza.

Aliongeza kuwa Wafanyabiashara hao wanaweza pia kuja nchini na kuwekeza mmoja mmoja au kwa kuungana na serikali kwa njia ya ubia na hivyo kusaidia uendelezaji wa maeneo ya utalii kwa faida ya pande zote mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news