NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezindua rasmi Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini Vienna nchini Austria.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Naibu Waziri wa Austria anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal wakinyanyua mikono baada ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna, Austria.
Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo ni mafanikio yanayoimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Vienna na kinaonesha jinsi Tanzania inavyoipa kipaumbele Austria.
Mhe. Dkt. Tax akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna Austria.
“Kufunguliwa kwa Ubalozi huu ni mafanikio makubwa ambayo yanaimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo hapa jijini Vienna na kinaonesha kwa vitendo kuwa Tanzania inaipa kipaumbele Uhusiano wake na Austria,” alisema Dkt. Tax.

Kaimu Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Vienna nchini Austria Bi. Elizabeth Rwitunga akizungumza katika hafla ya kuzindua Ubalozi wa Tanzania Vienna terehe 12 Juni, 2013.

“Austria inapongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake Austria na hivyo kuungana na nchi nyingine 16 za Afrika ambazo zina Balozi zao hapa nchini, niwa ahidi na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Austria iko tayari kuusaidia Ubalozi huo kwa kila hali ili ufikie malengo ya kuanzishwa kwake,”alisisitiza Waziri huyo.
Baadhi ya wanadiplomasia waliopo jijini Vienna walioshiriki hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna wakifuatilia ufunguzi huo.