TRA yatoa mwaliko elimu mifumo ya usimamizi kodi ya zuio iliyoboreshwa

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mwaliko wa mafunzo ya matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa kodi ya zuio iliyoboreshwa (upgraded withholding tax management systems).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 2, 2023 na uongozi wa mamlaka hiyo imefafanua kuwa, TRA kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango itatoa mafunzo hayo Juni 6, 2023 mkoani Dodoma kwa walipakodi walio katika kundi la taasisi za umma nchini.

"TRA kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango tunapenda kuwajulisha walipakodi walio katika kundi la taasisi za umma nchini kuwa, itafanya mafunzo maalum ya matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa kodi ya zuio (withhloding tax) kufuatia maboresho yaliyofanyika hivi karibuni.

"Semina hii itafanyika siku ya Jumanne ya Juni 6, 2023 mkoani Dodoma katika Ukumbi wa African Dream Hotel kuanzia saa 3:00 asubuhi na itaendeshwa na TRA Makao Makuu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango," imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo walipa kodi walio katika kundi hilo wanahimizwa kushiriki mafunzo hayo ili kujijengea uwezo wa kutumia mifumo hiyo kwa ufasaha na kuziwezesha taasisi kutimiza matakwa ya sheria na taratibu zinazosimamia utozaji wa kodi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news