UCHUNGUZI WA KIIKOLOJIA KUHUSU UGONJWA WA VIRUSI VYA MARBURG WAANZA KAGERA

NA MWANDISHI WETU

WATAALAMU kutoka Wizara za kisekta chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameanza uchunguzi wa Kiikolojia kuhusu Ugonjwa wa Virusi vya Marburg baada ya ugonjwa huo kutokomezwa nchini.
Mkurugenzi Msaidizi Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Prudence Costantine akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Ziara ya kufanya uchunguzi wa kiikolojia ili kubaini uwepo wa Wanyama wanaoweza kuhifadhi Virusi vya Marburg na mwingiliano wao na wanadamu katika Mkoa wa Kagera.

Wataalamu wanaounda timu wanatoka ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ofisi ya Waziri Mkuu ( Menejimenti ya Maafa), Wizara ya 

Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori (TAWIRI), na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI).
Baadhi ya Wataalamu waliopo kwenye ziara hiyo.

Watalam hao ambao wamekutana Mkoani Kagera wanalenga mufanya uchunguzi wa kiikolojia ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kimataifa ya kufanyika kwa shughuli mbalimbali za ufuatiliaji baada ya ugonjwa huo kutoweka.

Mkurugenzi Msaidizi Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Prudence Constantine amesema Ofisi ya Waziri Mkuu imeratibu sekta na Taasisi mbalimbali kufanya uchunguzi wa kiikolojia ili kubaini uwepo wa Wanyama wanaoweza kuhifadhi Virusi vya Marburg na mwingiliano wao na wanadamu ambapo Uchunguzi huu ni moja kati ya juhudi za pamoja za kuendelea kujua chanzo cha tatizo, kujiandaa, kukabiliana na dharura za kiafya ikiwemo endapo zitajitokeza.
Baadhi ya Wataalamu waliopo kwenye ziara hiyo.

"Wizara ya Afya imeainisha uchunguzi huu kati ya kazi muhimu zinazotakiwa kufanyika ndani ya mpango wa siku 90 wa kurejesha hali Mara baada ya mlipuko wa Marburg ulipotangazwa kuisha,"ameeleza Mkurugenzi Prudence.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt. Issessanda Kaniki akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera wakati wa Ufunguzi wa ziara hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera,Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Issessanda Kaniki amesema baada ufuatiliaji wa mbinu za utafiti na vipimo ndani ya siku 42 tumeweza kuudhibiti ugonjwa huo hivyo hadi sasa hakuna Mgonjwa hata mmoja.

"Baada ya Ufuatiliaji lakini pia na mbinu mbalimbali za Utafiti Mkoa wa Kagera pamoja na Nchi tunazopakana nazo kwa sasa mlipuko wa Ugonjwa wa Marburg haupo tena,"amesema Dkt.Kaniki.
Mkurugenzi Msaidizi Tiba na Mratibu Tafiti Wizara ya Afya, Dkt. Pius Horumpende akitoa muongozo kuhusu ziara hiyo.

Uchunguzi huu wa Kiikolojia utakaofanyika kati ya tarehe 12 na 24 Juni, 2023 utahusisha uchukuaji wa sampuli za Wanyamapori, wanyama wa kufugwa pamoja na kufanya utafiti shirikishi jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Muleba na Kyerwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news