NA DIRAMAKINI
WAKILI Mkuu wa Serikali, Dkt.Boniphace Nalija Luhende amesema,miaka mitano tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo imepiga hatua kubwa ikiwemo usimamizi wa mashauri ya madai na usuluhishi kwa ufanisi mkubwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Jarida Maalum la Miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kulizindua kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 5, 2023. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt boniface Luhende na kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Dkt.Luhende ameyasema hayo leo Juni 5, 2023 jijini Dodoma mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
"Sherehe hizi za leo ni muhimu sana kwani tangu kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali tarehe 13 Februari 2018, kwa mara ya kwanza leo tumeweza kukutana na wadau wetu mbalimbali tukitathmini tulipotoka, tulipo na tunapoelekea.
"Ninachukua fursa hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, pamoja na wewe binafsi Mhe. Waziri Mkuu kwa kazi kubwa mnayoendelea kuifanya katika kuiletea nchi yetu maendeleo.
"Hasa katika kipindi hiki cha mdororo wa uchumi wa dunia ambapo Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati nchi nzima ikiwamo ujenzi wa miundombinu mikubwa ya barabara, Reli ya Kisasa ya SGR, ujenzi wa bwawa la Nyerere na miradi mingine mbalimbali."
Dkt.Luhende amebainisha kuwa,maadhimisho hayo yanahusisha mabanda ya maonesho kwa ajili ya kuelimisha umma masuala mbalimbali ya kisheria na mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali zaidi ya 600 kutoka taasisi mbalimbali za umma.
Lengo likiwa ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo mawakili hao katika masuala mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa weledi mkubwa zaidi.
"Mafunzo haya yatafanyika kuanzia Juni 6, 2023 hadi Juni 8, 2023 ambapo wakufunzi wabobevu 24 ambao ni Majaji na Majaji wastaafu kutoka Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu ya Tanzania, wataalam wabobezi wa Sekta ya Sheria nchini, wakufunzi kutoka vyuo vikuu hapa nchini watatoa mada mbalimbali kwa mawakili tajwa kuhusu masuala ya sheria ikiwemo uandaaji na usimamizi wa mikataba, masuala ya uwekezaji, mafuta na gesi, na usuluhushi wa migogoro kwa njia ya majadiliano."
Amesema,ili kuboresha huduma za kisheria katika sekta ya umma, mnamo tarehe 13 Februari, 2018, Serikali ilifanya maboresho katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuiwezesha kutoa huduma bora za kisheria kwa sekta ya umma.
Kwa mamlaka aliyonayo chini ya Ibara ya 36 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitoa “Amri ya Maboresho ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali” kupitia Tangazo la Serikali Na.48 la mwaka 2018 [Office of the Attorney-General (Re-structure) Order, 2018. (GN.No. 48 of 2018)].”
Dkt.Luhende amefafanua kuwa, amri hiyo ya maboresho ilitambua kuwepo kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Kufuatia mabadiliko haya,Februari 13, 2018, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilianzishwa kupitia Hati Idhini (Instrument) ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 50 la Mwaka 2018 [The Office of the Solicitor General (Establishment Order) 2018].
Kwa mujibu wa muundo wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali,Dkt.Luhende amefafanua kuwa, Wakili Mkuu wa Serikali ndiye Mkuu wa taasisi akisadiwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Afisa Masuuli na Mamlaka ya Nidhamu kwa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Idara
Dkt.Luhende amefafanua kuwa, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inaundwa na idara tano ikiwemo Idara ya Madai: yenye vitengo vya Madai ya Ndani, Madai ya Nje na Madai ya Kikatiba, Haki za Binadamu na Uchaguzi.
Pia kuna Idara ya Usuluhishi: yenye vitengo vya Usuluhishi wa Kitaifa na Usuluhishi wa Kimataifa. Idara ya Usimamizi wa Mashauri na Udhibiti Ubora: yenye vitengo vya Uratibu na Usimamizi wa Mashauri na Udhibiti Ubora. Idara ya Utawala yenye sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu na Idara ya Mipango yenye sehemu ya Mipango na Bajeti na Ufuatiliaji na Tathmini.
Pia, amesema, ofisi hiyo ina vitengo saba vya Uhasibu na Fedha; Ukaguzi wa Ndani; Ugavi na Manunuzi; Masjala ya Sheria; Maktaba na Utafiti; TEHAMA; na Mawasiliano Serikalini.
"Lengo mahsusi la kuanzishwa kwa ofisi lilitokana na nia ya Serikali kuwa na ofisi moja inayowajibika na shughuli zote za kila siku za uratibu,ushauri na uendeshaji wa mashauri ya Madai na Usuluhishi kwa niaba ya Serikali Kuu, Idara zinazojitemea, Mashirika ya Kiserikali na Serikali za Mitaa ndani na nje ya nchi.
Aidha, amesema Aprili 14, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimteua Dkt.Julius Clement Mashamba kuwa Wakili Mkuu wa Serikali na Dkt. Ally Saleh Possi kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.
"Mheshimiwa Mgeni Rasmi, mnamo tarehe 15 Agosti 2018 ulishiriki ukiwa Mgeni Rasmi katika kuzindua Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
"Leo, unashuhudia Ofisi ya Wakili Mkuu ikiwa imetimiza miaka mitano, ni jambo la faraja sana kwetu sisi sote kuwa nawe hapa.
"Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Amri ya Kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imebainisha majukumu mengi ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali."
Majukumu
Dkt.Luhende amefafanua kuwa,baadhi ya majukumu hayo ni kuendesha na kusimamia mashauri yote ya madai, mashauri ya haki za binadamu na kikatiba na mashauri ya usuluhishi yanayoihusu Serikali;
Kutoa mwongozo kwa Wanasheria na Mawakili wa Serikali ambao watasimamia uendeshaji wa mashauri ya madai, mashauri ya haki za binadamu na kikatiba na mashauri ya usuluhishi yanayoihusu Serikali;
Majukumu mengine ni kuandaa na kufungua mashauri mbalimbali kwenye Mahakama na Mabaraza ya Usuluhishi kwa niaba ya Serikali;
Kutoa ushauri kwa Serikali na kuratibu mwenendo wa mashauri ya Serikali yaliyopo Mahakamani na Mabaraza ya
Usuluhishi ndani na nje ya Tanzania;
Sambamba na kutunza kumbukumbu za mashauri au kesi zote za Serikali zinazosimamiwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Dkt.Luhende amebainisha awali kabla ya kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, mashauri ya Madai na Usuluhishi yaliendeshwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali chini ya Idara ya Madai na Usuluhishi (Division of Civil Litigation and Arbitration (DLA) wakati Mashauri ya Kikatiba na Haki za Binadamu yaliendeshwa na Idara ya Katiba na Haki za Binadamu.
Katika kipindi hicho, amesema baadhi ya taasisi za Serikali zilikuwa zikiwasilisha mashauri yao ili yaweze kuendeshwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku Taasisi nyingine za Serikali zikiendesha mashauri kupitia Mawakili wa Taasisi ‘in house lawyers’ pamoja na Mawakili wa kujitegemea.
Vilevile mashauri ya Kimataifa yaliendeshwa na Mawakili binafsi. Utaratibu huo ulikuwa unaigharimu Serikali kiasi kikubwa cha fedha za kuwalipa Mawakili binafsi.
Pia, mfumo uliokuwepo haukuweza kuwajenga kitaaluma Mawakili wa Serikali ili kuendesha mashauri makubwa na ya kimataifa na wakati mwingine, taarifa nyeti za Serikali zilivuja kirahisi kupitia kesi hizo.
Aidha, kutokana na mfumo duni wa usimamizi wa mshauri, Dkt.Luhende amesema kuna baadhi ya kesi ambazo zilikuwepo Mahakamani zilipoteza mwelekezo na ufuatiliaji wake ulikuwa mgumu.
"Kwa sababu ya kukosekana kwa mfumo mzuri wa uratibu, ilikuwa ni kawaida kwa kesi kusililizwa upande mmoja
ambapo mara nyingi hukumu zilizotoka ziliingizia Serikali hasara.
"Mheshimiwa Mgeni Rasmi,Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inatambua matarajio ya Serikali na taasisi zake na tunaahidi kuwa tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha tunatekeleza majukumu hayo na kufikia matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Hivyo, napenda kuwahakikishia wadau wetu wote kuwa, tutaendelea kufanya kazi hiyo kwa weledi na uadilifu mkubwa na kutekeleza ipasavyo malengo ambayo kwayo ilianzishwa.
"Mheshimiwa Mgeni Rasmi,matunda ya kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yameanza kuonekana dhahiri ndani ya Serikali.
"Matunda hayo ni pamoja na Serikali kuwa na uwakilishi wa uhakika na usio na gharama kubwa katika kuendesha kesi za madai na usuluhishi zinazoihusu Serikali ndani na nje ya nchi."
Mafanikio
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt.Luhende amefafanua kuwa, baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka mitano kutokea kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni Usimamizi wa Mashauri ya Madai na Usuluhishi.
Amesema, hadi kufikia Mei 31, 2023,ofisi hiyo imeendesha jumla ya mashauri 7,162 ikiwemo mashauri 7,025 ya madai na mashauri 137 ya usuluhishi.
Dkt.Luhende amesema, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 hadi Aprili 30, 2023, ofisi ilimaliza mashauri ya madai 518 kati ya mashauri hayo mashauri 45 yaliisha kwa njia ya majadiliano.
"Ofisi pia ilimaliza mashauri ya usuluhishi 15 kati ya mashauri hayo sita yaliisha kwa majadiliano. Hivyo, kuokoa shilingi bilioni 305.41 kwa mashauri ya madai na shilingi trilioni 7.26 kwa mashauri ya usuluhishi na kufanya fedha zote zilizookolewa kuwa shilingi trilioni 7.57.
"Fedha hizi zilipaswa kulipwa na Serikali kwa wadai endapo ingeshindwa mashauri husika kwenye Mahakama na Mabaraza ya Usuluhishi."
Vilevile, Dkt.Luhende amebainisha kuwa, ofisi hiyo imeongoza na kushiriki katika Timu za Serikali za Majadiliano (GNT) na kufanikisha kumaliza mashauri au migogoro mbalimbali kwa njia ya majadiliano, usuluhishi na maridhiano nje ya Mahakama kwa mafanikio makubwauimarisha Mifumo ya Usimamizi wa Mashauri na Udhibiti wa Ubora.
Pia, amesema katika kipindi cha miaka mitano, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imeimarisha mfumo wa kukusanya takwimu za mashauri, kufanya ufuatiliaji wa mienendo ya mashauri na kupitia sheria zinazohusu mashauri ya madai na usuluhishi.
Skt.Luhende ameendelea kubainisha kuwa,ofisi hiyo imeweza kuandaa miongozo ya kusimamia na kudhibiti viwango vya ubora vya Mawakili katika uendeshaji wa Mashauri (Civil Litigation and Arbitration Practice Directions, 2021 and Quality Assurance Manual, 2021).
Vile vile, Ofisi imeweza kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client Service Charter) ambao unaiwezesha Ofisi ya Wakili Mkuu kuweka aina ya huduma, viwango, ubora, haki na wajibu wa mteja na utaratibu unaotumika kutoa huduma kwa wadau ikiwemo Serikali na taasisi zake,sekta binafsi na wananchi na namna ya kupata mrejesho.
Bajeti
Wakati huo huo, Dkt.Luhende ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuongeza bajeti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Katika mwaka wa Fedha 2018/19 Ofisi ilipata Bajeti ya Shilingi bilioni 4.17, Shilingi bilioni 7.29 kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020;shilingi bilioni 11.48 kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021, Shilingi bilioni 12.13 kwa Mwaka wa Fedha 2021/22, Shilingi bilioni 12.81, Mwaka wa Fedha 2022/23 na kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 Ofisi imepatiwa bajeti ya Shilingi bilioni 17.07 sawa na ongezeko la asilimia 25 ukilinganisha na bajeti ya Mwaka 2022/23.
Dkt.Luhende amefafanua kuwa, kuongezeka kwa bajeti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kumeiwezesha Ofisi kutekeleza majukumu yake ya msingi ya usimamizi na uendeshaji Mashauri ya Madai na Usuluhishi kwa niaba ya Serikali kwa ufanisi na kupunguza changamoto zinazotokana na ufinyu wa bajeti uliokuwepo hapo awali.
Ofisi
Aidha, Dkt.Luhende amebainisha kuwa, ilii kupeleka huduma karibu na taasisi na Ofisi za Serikali zilizoko katika
mikoa husika pamoja na wananchi,ofisi ina jumla ya Ofisi 17 katika mikoa yenye Masjala ya Mahakama Kuu.
Mikoa hiyo ni pamoja na Dar es salaam, Morogoro, Tanga, Dodoma, Mbeya, Iringa, Rukwa, Ruvuma,Tabora, Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Kagera, Kilimanjaro, Arusha,Mara na Mtwara. Katika Mwaka ujao wa Fedha 2023/2024 na wanatarajia kufungua Ofisi katika Mkoa wa Manyara.
Ajira
Wakati Ofisi inaanzishwa mwaka 2018, Dkt.Luhende amefafanua kuwa, ilikuwa na watumishi 37 waliohama kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi nyingine za Serikali.
Kati ya watumishi hao 37, amesema watumishi 27 walikuwa ni mawakili wa Serikali. Hadi kufikia Mei 31, 2023, ofisi ina watumishi 232 wakiwemo Mawakili wa Serikali 128.
Aidha, Ofisi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 amesema, imetenga bajeti ya kuajiri watumishi wapya 40 ikiwemo mawakili 29.
Mafunzo
Dkt.Luhende amefafanua kuwa,ofisi imeendelea kuwajengea uwezo watumishi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi ikiwemo mafunzo ya kiubobevu katika maeneo maalum, katika mwaka wa fedha 2022/23 jumla ya watumishi 27 wamepewa ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu na watumishi 28 walipewa ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi ndani na nje ya nchi.
Pia, amesema ofisi imetoa mafunzo kwa viongozi (Menejimenti) ili kuweza kuwakumbusha mambo ambayo wanapaswa kuyafanya na kuyaishi kama viongozi.
Makao makuu
Katika hatua nyingine, Dkt.Luhende amesema, Julai 25,2022 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilianza ujenzi wa jengo la Makao Makuu yake katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma lenye ukubwa wa mita za mraba 17,342 unaotarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 26.2 kama gharama za mkandarasi na kiasi cha shilingi milioni 497.7 kama gharama ya Mshauri Mwelekezi.
Amesema, ujenzi huo unategemewa kukamilika Januari 24, 2024 ambapo kama ukikamilika utaiwezesha ofisi kuwa na jengo lenye jumla ya ghorofa tano.
Vituo jumuishi
Aidha, Dkt.Luhende amesema, ofisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, zinashirikiana katika utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa Vituo Jumuishi vya taasisi za sheria kwa lengo la kusogeza huduma za kisheria na utoaji wa haki karibu na wananchi.
Sambamba na hilo, amesema Novemba, 2022 ofisi ilishiriki uzinduzi wa ujenzi wa jengo jumuishi la taasisi za kisheria jijini Mwanza.
Magari
Dkt.Luhende amesema, katika kipindi cha miaka mitano, Ofisi ya Wakili Mkuu imeweza kununua magari mapya 23 na kufanya ofisi kuwa na jumla ya magari 31.
Kuongezeka kwa idadi ya magari kumesaidia kuwa na usafiri wa uhakika ambao unarahisisha utekelezaji wa majukumu ya kiofisi na pia kuwahakikishia usalama watumishi pamoja na nyaraka za Serikali ambazo wanalazimika kuwa nazo wakati wanaenda Mahakamani.
Aidha,katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 Ofisi ya Wakili Mkuu imetenga bajeti kwa ajili ya kununua magari mengine matatu ambayo itafanya kuwa na jumla ya magari 34.
Ushiriki
Dkt.Luhende amefafanua kuwa,katika kipindi cha miaka miwili ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan,ofisi imeendelea kuboresha mifumo mbalimbali ya TEHAMA ikiwemo mfumo wa kuhifadhi nyaraka za Maktaba (OSG e-library), mfumo wa usimamizi wa mashauri na matengenezo ya vifaa vya TEHAMA na kuweza kununua vifaa vya kufanyia mikutano kwa njia ya masafa ya video (Video Conference).
Pia,ofisi imeendelea kuelimisha na kuhabarisha umma kwa kutoa taarifa mbalimbali za Ofisi ya Wakili Mkuu kwa wadau na wananchi kwa ujumla ikiwemo uchapishaji wa nakala 2,250 za Jarida la Wakili Mkuu;makala 120; machapisho na vipeperushi 750; vipindi maalum vitatu vya runinga; mabango ya mtandaoni 25; na kuchambua na kuweka taarifa za Ofisi kwenye tovuti ya Ofisi (www.osg.go.tz:) na mitandao ya kijamii.
"Mheshimiwa Mgeni Rasmi,ukirejea mafanikio haya yaliyoelezwa, ni dhahiri kuwa malengo ya kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yameweza kufikiwa ndani ya kipindi kifupi tu cha miaka mitano licha ya kuwepo kwa
changamoto mbalimbali ambazo Serikali imeendelea kuzishughulikia."
Changamoto
Dkt.Luhende amefafanua kuwa, changamoto hizo ni pamoja na baadhi ya taasisi za umma kutokuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo wakati wa kuwachukulia hatua za kinadhimu watumishi wa umma, hivyo kupelekea kufunguliwa kwa mashauri mengi ya kazi ambayo yangeweza kuepukwa endapo taratibu na sheria zingezingatiwa.
Pia, amesema changamoto nyingine ni ukosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wizara na taasisi za Serikali. "Baadhi ya Taasisi za Serikali kutoa ushirikiano hafifu na kwa wakati katika kuandaa nyaraka mbalimbali zinazohitajika mahakamani."
Dkt.Luhende amefafanua kuwa, migogoro mingi ya ardhi imetokana na tasisisi zinazosimamia sekta ya ardhi kutozingatia taratibu za utwaaji wa maeneo na upimaji wa viwanja, malipo ya fidia na ugawaji wa viwanja.
"Mwingiliano utoaji wa leseni kati ya wizara na taasisi za umma.Mfano, katika shauri moja lililohusisha Mkataba wa Utafutaji Mafuta na Gesi. Wizara ya Madini ilitoa leseni ya utafutaji madini, katika eneo ambalo tayari kampuni nyingine ya kigeni ina leseni ya utafutaji wa mafuta na gesi inayosimamiwa na Wizara ya Nishati."
Usimamizi hafifu wa mradi
Dkt.Luhende amefafanua kuwa,katika shauri moja Kampuni ya Utafutaji Mafuta na Gesi haikutimiza wajibu na majukumu yake ya kimkataba, hususani jukumu la kuchoronga kisima, lakini Serikali haikuchukua hatua zozote hadi pale mwekezaji alipovunja Mkataba na kuishtaki Serikali.
Jambo lingine, Dkt.Luhende amesema ni ucheleweshwaji wa kufanyia kazi malalamiko ya wawekezaji. Amesema,katika baadhi ya kesi,wawekezaji wamelalamika kuhusu mamlaka za Serikali kuandikiwa barua kadhaa za malalamiko mbalimbali.
Hata hivyo,amesema mamlaka za Serikali zimekuwa hazitoi majibu kwa wakati na pengine hazijibu kabisa. "Jambo hili lilisababisha wawekezaji kufungua shauri kutokana na kukosa ushirikiano na majibu ya hoja mbalimbali."
Pia amesema, jambo lingine ni kutoshirikisha Ofisi ya Mwasheria Mkuu."Baadhi ya taasisi za Serikali kuvunja Mikataba bila kushirikisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hivyo kushindwa kufuata taratibu za kuvunja
mikataba na kupelekea Serikali kushitakiwa katika Mahakama na Mabaraza ndani na nje ya nchi."
Kuchelewesha malipo kwa watoa huduma na wakandarasi, jambo hili Dkt.Luhende amesema,baadhi ya taasisi za umma huchelewa kufanya malipo kwa wakandarasi na watoa huduma kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa bajeti iliyotengwa wakati Mkataba ulipoingiwa au kuchelewa tu kwa maamuzi ya malipo na hilo
linasababisha Serikali kudaiwa deni, riba pamoja na gharama za kuendesha kesi.
Aidha, amesema changamoto nyingine ni uwezo mdogo wa wakandarasi na wawekezaji. "Kuna baadhi ya miradi, wawekezaji, watoa huduma na wakandarasi wanaopewa kuendesha huwa hawana uwezo wa kutosha na hivyo kukwama katika utekelezaji.
"Hii inatokana na kutofanyika upembuzi wa kina kuhusu uwezo wa wakandarasi hao. Wakandarasi hawa hukimbilia
mahakamani."
Katika hatua nyingine, Dkt.Luhende amebainisha kuwa, kwa upande wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali bado kuna
changamoto ya ufinyu wa bajeti.
"Kwa mfano, katika mwaka wa fedha 2022/23 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilipewa asilimia 63 ya kiasi kilichoombwa licha ya kuwa na ongezeko la watumishi 66 kutoka watumishi 177 mwaka 2021/22 hadi watumishi 243 katika mwaka wa fedha 2022/23.
"Kwa mwaka wa fedha 2023/24 ofisi ilipeleka maombi ya bajeti ya shilingi bilioni 23.58. Hata hivyo, Ofisi iliidhinishiwa shilling bilioni 17.07 sawa na asilimia 72 ya kiasi kulichoombwa.
"Jambo linaloleta changamoto katika uendeshaji wa mashauri kwa ufanisi, mafunzo ya weledi kwa Mawakili wa Serikali, vyombo vya usafiri, vifaa vya TEHAMA ikiwemo vifaa vya kuwezesha mikutano ya mitandao (video conference)."
Maslahi
Dkt.Luhende akizungumzia kuhusu maslahi kwa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali amesema,hayaendani na uzito wa majukumu ya ofisi.
"Jambo limeendelea kufanyiwa kazi na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Katika kukabiliana na changamoto kama zilivyoainishwa,ofisi inashauriwa yafuatayo.
"Mosi,taasisi za umma zikumbushwe kuzingatia sheria na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo usimamizi wa mikataba na kuvunja mikataba.
"Pili, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iendelee kutoa elimu na miongozo kwa taasisi za umma ili kuzingatia sheria na kanuni wakati wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wa umma.
"Tatu, taasisi zinazohusika na kusimamia wawekezaji, wasimamie kwa ukaribu zaidi utekelezaji wa miradi hiyo ili kuepusha madai makubwa kwenye maeneo ambayo mwekezaji hajawekeza vya kutosha.
"Nne, mikataba inayohusu uwekezaji ndani ya nchi na ile ya mashirikiano ya kiuwekezaji baina ya Tanzania na nchi nyingine (Bilateral Investment Trearty - BIT) ipitiwe kwa upya na nchi husika ziwe zinashirikishwa wakati mgogoro unapotokeana mwekezaji kutoka nchi yenye mkataba na Tanzania.
"Tano,kuwa na sehemu moja (one stop centre) ambayo mwekezaji atawasiliana na Serikali. Jambo hili litapunguza maelekezo tofauti na yanayokinzana kutoka Serikalini ambayo pengine yamekuwa yakitolewa na taasisi au idara mbalimbali kwa wawekezaji.
"Sita,kutunza nyaraka zote zinazotumika kwenye mawasiliano na wawekezaji, ili kuepusha upotezaji wa taarifa na kutoa maelekezo ambayo yanakinzana.
"Saba,kutoa elimu kwa watumishi wa umma kuhusu usimamizi wa mikataba, ili kujenga uwezo wa kusimamia kwa umakini zaidi mikataba na miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi.
"Nane,kufanya ukaguzi wa kina kabla ya Mwekezaji kuanza shughuli za kuomba kufanya uwekezaji, ikiwa ni pamoja na kujua iwapo anao uwezo, uzoefu wa uwekezaji anaotaka kuufanya nchini.
"Tisa,ombi letu kwa Serikali kuongeza wigo wa bajeti (ceiling) ya kawaida na ya maendeleo ili kuweza kutoa huduma stahiki na kuboresha mazingira ya kazi.
"Pia kuendelea kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali kwa kuwapatia mafunzo ya uendeshaji mashauri kwenye maeneo ya kimkakati kama vile uwekezaji, madini, mafuta na gesi na kuhakikisha kuwa tunawatumia Mawakili wa ndani kuendesha kesi zote za ndani na nje ya nchi pale ambapo sheria zinaruhusu kufanya hivyo,"amefafanua Dkt.Luhende.
Shukurani
Mbali na hayo, Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt.Luhende amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuiamini ofisi hiyo na kuwawezesha kwa hali na mali kwa kutoa
kipaumbele kwa mahitaji ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kadri inavyowezekana.
"Pia niwashukuru viongozi wakuu wa Serikali, Mhe. Makamu wa Rais Dkt.Isdory Mpango na wewe mwenyewe Mhe. Waziri Mkuu, kwa kumshauri Rais wetu vema na kwa uongozi madhubuti ambao umeleta amani na ustawi wa nchi.
"Naushukuru Wizara ya Katiba na Sheria, chini ya uongozi mahiri wa Dkt.Damas Ndumbaro na Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo, kwa kushirikiana na ofisi hii kwa ukaribu huku mkitoa maelekezo ya mara kwa mara pale
panapohitajika.
"Ninamshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt Jaji Eliezer Mbuki Feleshi kwa kuendelea kutoa miongozo mbalimbali kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na kusimamia mashauri ya serikali vema.
"Namshukuru sana Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi.Sarah Duncan Mwaipopo kwa kuendelea kusimamia majukumu ya ofisi hii kwa weledi na uaminifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kunishauri vema.
"Pia, ninaishukuru menejimenti na watumishi wote wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa kuendelea kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali vema, kwa ueledi na kwa uadilifu mkubwa huku wakiweka
maslahi ya Taifa mbele.
"Nawashukuru sana Viongozi waliotangulia kutumika katika Wizara yetu ya Katiba na Sheria, Ofisi hii na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao waliweka msingi wa ofisi hii.
"Napenda kumshukuru kipekee Mhe.Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb) aliyekuwa Waziri
wa Katiba na Sheria kipindi Ofisi hii inaanzishwa pamoja na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Lubango Kilangi.
"Kipekee nawashukuru Dkt Clement Julius Mashamba na Mhe.Jaji Gabriel Pascal Malata pamoja na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt Ally Possi kwa misingi waliyoiweka ambayo tunaendelea kuijenga na kuiboresha.
"Ninapenda pia kuwashukuru sana wadau wetu, Wizara na Taasisi za Serikali, Mahakama, Bunge, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma, Viongozi wa Dini, Vyama vya Kitaaluma ikiwemo Chama cha Mawakili wa Serikali (Public Bar Association), Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mawakili wa Serikali, Mawakili wa Kujitegemea na wadau wengine wote kutoka Sekta ya umma na binafsi kwa kuendelea kushirikiana nasi katika maeneo mbalimbali,"amefafanua Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Luhende.