VIDEO:Dkt.Gustavus Deusdedith ataja sababu za kufungua kiwanda cha nguo Dodoma

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mtendaji wa Taven Industries Company Limited,Dkt.Gustavus Deusdedith amesema, nia ya kuanzisha kiwanda hicho ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa nguo za aina mbalimbali nchini ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Kiwanda hicho kilichopo Block D, Plot 716, Chihoni Kata ya Nala jijini Dodoma,licha ya kuunga mkono jitihada hizo kimetoa fursa za ajira kwa Watanzania mbalimbali.

"Nia nzima ya uanzishwaji wa kiwanda hiki cha nguo ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita hasa katika Sera ya Viwanda na hivyo kuongeza upatikanaji wa bidhaa hapa hapa nchini na sio kutoka nje ya nchi.

"Tunaunga mkono Serikali yetu ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sera ya uzalishaji ambayo imekuwa ikinadiwa kwa miaka kadhaa. Sasa nasi, tumeona tuingie katika eneo hilo,"amefafanua Dkt.Deusdedith.

 HUDUMA ZETU

Uzalishaji na usambazaji wa 

1 T-shirt za aina zote

- Za kola (polo)

-Za round

- Zenye shingo v

2. Sare za aina zote 

-Za shule

-Za hoteli, viwanda na maeneo ya kazi, biashara na ulinzi

3.Nguo za mitindo mbalimbali

-Tunazalisha kwa mteja aliyeandaa mitindo au sampuli

-Leta nguo ya sampuli au mchoro

-Nguo za watoto

-Nguo za safari

-Nguo za kutokea

-Nguo za kiofisi na sehemu rasmi

-Na mitindo yote iliyoandaliwa au kuandaliwa na wataalamu wetu

4. Huduma za uchapishaji wa nguo kwa njia ya

-Kudarizi

-kuchapa kwa njia ya wino na moto na michoro ya asili

5 Ushauri na uelekezi

Mawasiliano

0716041476

0717514324

0715094290

AU

Jibu kwa kubonyeza namba ya huduma unayotaka ili kupata maelekezo zaidi mfano 1

Tembelea youtube channel yetu

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news