WANANCHI TEGERUKA, MUGANGO WAMSHUKURU RAIS DKT.SAMIA KWA MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.75/-

NA FRESHA KINASA

WANANCHI wa Kata ya Tegeruka na Mugango katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa mradi wa maji ya bomba ambao utakuwa mwarobaini katika kutatua tatizo la maji na kuchochea shughuli zao za kimaendeleo. 
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani humo.

Wamesema, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kufanya juhudi nyingi za dhati za maendeleo jimboni humo ambazo zinawaneemesha ikiwemo miradi ya maji. 

Miongoni mwa juhudi hizo, ni utekelezaji wa mradi wa maji ya bomba ya kata za Tegeruka na Mugango unaogharimu Shilingi Bilioni 4.75 ambao utatatua tatizo za maji safi na salama na kuchangia maendeleo yao ya kiuchumi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Juni Mosi, 2023 imeeleza kuwa, vifaa vya mradi huo vimeanza kununuliwa. 

Taarifa hiyo imeeleza kwamba, "kata hizi mbili zitapata maji Kutoka bomba la Mugango-Kiabakari- Butiama."

"Tunashukuru Wizara ya Maji na MUWASA kukamilisha taratibu zote za Mkandarasi kuanza kazi."

"Mradi huu ni wa thamani ya shilingi Bilioni 4.75 tunaendelea kumshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo mazuri kuhusu matumizi ya maji ya Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news