NA MWANDISHI WETU
WATAALAMU 132 wamepatiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji mkubwa (Highly Dependent patients) yaliyotolewa na wauguzi bobezi wa wagonjwa mahututi (Critical care nurse specialist) na Madaktari bobezi wa mahututi.
Katika hatua nyingine madaktari na wauguzi 40 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambao wanahudumia wagonjwa Mahututi wamepatiwa mafunzo ya kuboresha huduma katika maeneo ya kuzuia na kudhibiti maambukizi (IPC) , namna ya kutambua viashiria hatarishi na kuchukua hatua za haraka kwa kuwasaidia wagonjwa pamoja na kubadilisha mitazamo kwa watoa huduma.
Mafunzo hayo ya siku nne yaliendeshwa na wataalamu wawezeshaji kutoka Kitengo cha Ubora wa Huduma (Quality assuarance) Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ufadhili wa EMORY University na ABBOT Fund.