NA DIRAMAKINI
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Balozi Dkt.Pindi Hazara Chana (Mb) kwa mamlaka aliyonayo katika Kifungu cha 10 cha Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (Sura ya 49) amefanya mabadiliko katika nafasi ya Msajili wa Vyama vya Michezo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 19, 2023 na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo,Bw.Eleuteri E.Mangi, lengo la mabadiliko hayo ni kuboresha utendaji kazi katika sekta ya michezo nchini.

Mheshimiwa Waziri amemteua, Bw.Evordy Eliezer Kyando kuwa Kaimu Msajili wa Vyama vya Michezo nchini kuchukua nafasi ya Bw.Riziki Juma Majala.
Aidha, kwa mujibu wa tarifa hiyo kabla ya uteuzi huo, Bw.Evordy Eliezer Kyando alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.