NA SHAMIMU NYAKI
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Juni 2, 2023 amewasili katika Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Algers nchini Algeria na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo , Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu ikiwa ni maandalizi ya kushuhudia mchezo wa Fainali ya Pili ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Dar es Salaam Young Africa (Yanga) na USM Alger ya nchini humo utakaochezwa Juni 3, 2023 majira ya saa 2: 00 usiku ambazo ni saa za nchi hiyo.



Katika ziara hiyo Mhe. Chana ameambata na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid, Mwenyekiti UWT Taifa Mhe. Mary Chatanda, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ndg. Nicholas Mkapa, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Wallace Karia, baadhi ya Waheshimiwa Wabunge na mashabiki.