Waziri Dkt.Gwajima atoa maagizo kwa wataalamu kuhusu Jukwaa la Kizazi chenye Usawa (GEF)

NA MWANDISHI WETU
WMJJWM, MOROGORO

WATAALAMU wabobezi wa masuala ya jinsia wameagizwa kutambua masuala yaliyowekewa ahadi za nchi katika Jukwaa la Kizazi chenye Usawa (GEF) ili kutekeleza Programu ya Kizazi chenye Usawa kwa Ufanisi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa maelekezo hayo mkoani Morogoro leo Juni 22, 2023, wakati akifungua mafunzo kwa wataalamu hao walioteuliwa kusimamia utekelezaji wa ahadi hizo, zilizotolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza maazimio ya Mkutano wa Beijing kuelekea Kizazi chenye usawa. 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo kuhusu Programu ya Kizazi chenye usawa wakati akifungua mafunzo hayo Juni 22, 2023 mjini Morogoro.
Waziri Dkt. Gwajima amewataka Wataalamu hao kuratibu Afua zinazotekelezwa na sekta zao na kuzitolea taarifa kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwa na taarifa zenye athari chanya kwa sekta zao zitakazoonesha mazuri yaliyotekelezwa na kuimarisha mawasiliano miongoni mwao. 
"Katika utekelezaji wa programu ya nchi, majukumu yenu yatakuwa ni kuhakikisha masuala ya kizazi chenye usawa yanaingizwa katika mipango na bajeti zenu, kuandaa taarifa za utekelezaji wa maeneo husika, kutoa elimu ya masuala ya GEF kwa wadau, kuhakikisha kuna miongozo yenye kuzingatia masuala ya jinsia katika bajeti za wizara na taasisi zenu,"amesema Dkt.Gwajima.
Washiriki wa mafunzo ya utekelezaji wa Programu ya Usawa wa Kijinsia yanayofanyika mkoani Morogoro, wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Juni 22, 2023.
Amesema, lengo ni kufikia Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. Hivyo mafunzo hayo yanawajengea uwezo kuhusu Programu, Uratibu na utekelezaji ili kutekeleza malengo na ahadi zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ta Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wataalamu kutoka Wizara mbalimbali za kisekta, zinazotekeleza Programu ya Taifa ya Usawa wa kijinsia (GEF), Juni 22, 2023 mkoani Morogoro.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju amewataka wataalamu hao kuhakikisha wakitoka kwenye mafunzo hayo wanakwenda kuwa chachu ya utekelezaji wa programu hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la CARE International Prudence Masako akieleza lengo la mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa Wizara za kisekta katika utekelezaji wa Programu ya Kizazi chenye usawa(GEF) Juni 22, 2023 mkoani Morogoro.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Care International lililowezesha mafunzo hayo, Prudence Masako amesema, shirika hilo linaunga mkono jitihada za utekelezaji wa ahadi za nchi Rais Samia alipotoa ahadi hizo za kuhakikisha usawa wa kijinsia unafikiwa katika eneo la haki ya usawa wa kiuchumi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika picha ya pamoja na washiriki wa mafynzo ya utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye Jukwaa la Kizazi chenye usawa baada ya ufunguzi uliofanyika Juni 22, 2023 mkoani Morogoro. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wakili Amon Mpanju na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Jinsia Rennie Gondwe. Kulia kwake ni Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Care International Prudence Masako na Mkurugenzi wa huduma za Sheria Evelyne Makala.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM).

Programu hiyo ya kizazi chenye usawa itakayotekelezwa kwa miaka mitano (2021/22-2025/26), inatokana na ahadi ya Rais Mhe. Dkt. Samia katika utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Beijing, kwenye Jukwaa la Kizazi chenye usawa kwamba atahakikisha usawa wa kijinsia unafikiwa hasa katika eneo la Haki ya kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news