NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Stergomena Tax kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kituo cha Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) wameinadi Tanzania kama Kituo bora cha uwekezaji kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Italia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika mkutano na jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza katika mkutano na jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya a uwekezaji Zanzibar Bw. Khamis Mzee akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Dkt. Gilead Teri akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Waziri Tax amewaeleza Wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kurekebisha sera na sheria mbalimbali ili kuwafanya wawekezaji wawe na mazingira bora ya kuendesha shughuli zao na hivyo kuvutia wawekezaji wengi zaidi.
Wafanyabiashara hao wameelezwa kuwa Tanzania ni salama kwa wao kuwekeza mitaji yao, ambapo pia watakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kulifikia na kunufaika na soko kubwa la EAC, SADC na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).
Miongoni mwa sekta zilizowavutia Wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Kilimo, Utalii, Viwanda, Uchumi wa Buluu, na Ujenzi.
Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax akizungumza na mmoja wa Wafanyabiashara wa Italia wakati wa mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Mkutano huo uliofanyika jijini Roma, Italia ulijumuisha Wafanyabiashara waliowekeza nchi Tanzania katika Sekta mbalimbali na wenye nia ya kuwekeza nchini.