Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ipo katika Wiki ya Utumishi wa Umma

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo iliundwa Kupitia Tangazo la Serikali Na.782 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali la tarehe 22 Novemba, 2021. Katika kutekeleza majukumu yake kikamilifu, Wizara kimuundo imegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni:

i. Usimamizi na utekelezaji wa masuala ya kisekta

ii. Uendeshaji, uratibu na usimamizi

USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA KISEKTA

Eneo hili linatekelezwa na Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Idara ya Maendeleo ya Sanaa na Idara ya Maendeleo ya Michezo kwa ushirikiano na Taasisi zilizopo chini ya Idara hizo.

UENDESHAJI URATIBU NA USIMAMIZI

Eneo hili linatekelezwa na Idara ya Sera na Mipango, Idara ya Utawala na Rasilimali Watu,Kitengo cha Fedha na Uhasibu, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Kitengo cha Huduma za Sheria na Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Kuendeleza utambulisho wa Taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa Habari,Kukuza Utamaduni na Michezo kwa Maendeleo ya Jamii na Uchumi.

MAJUKUMU YA WIZARA

Ili kufanikisha majukumu yake Wizara inatekeleza Sera za Utamaduni na Michezo pamoja na Malengo yake.

SERA YA MAENDELEO YA UTAMADUNI YA MWAKA 1997

Malengo yake:

i. Kushirikisha shughuli za Utamaduni wa Taifa kuanzia Shule za Awali, Sekondari na Elimu ya Juu na kuhakikisha kwamba mafunzo ya Utamaduni yanaingizwa katika Mitaala na muhtasari na kufundishwa shuleni na vyuoni.

ii. Kuhimiza na kukuza utaifa kwa vijana wetu na wananchi kwa ujumla.

iii. Kuhimiza Utu katika Maendeleo ya Taifa.

iv. Kuimarisha Uchangiaji wa gharama, Ukuzaji, Utunzaji na Uimarishaji wa Taasisi za Utamaduni kwa watumiaji wa huduma hizo.

v. Kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Utamaduni na jinsi sanaa inavyoweza kutumika katika kupambana na UKIMWI.

SERA YA MAENDELEO YA MICHEZO YA MWAKA 1995

Malengo yake ni:

i. Kuhamasisha wananchi kushiriki michezo na mazoezi ya viungo vya mwili ili kuimarisha afya zao.

ii. Kuhakikisha timu na wachezaji wetu wanashiriki kikamilifu katika mashindano na michezo ya kitaifa na kimataifa.

iii. Kufanya utafiti wa Michezo ya Jadi kwa lengo la kuifufua na kuiendeleza.

iv. Kuimarisha ushirikiano na mataifa mengine katika utoaji wa elimu kwa michezo na wanamichezo.

v. Kusimamia ujenzi wa miundombinu ya kisasa katika Sekta ya Michezo.

vi. Kuimarisha Utawala bora katika michezo.

vii. Kutoa Mafunzo ya wataalamu wa michezo.

viii. Kupambana na Janga la UKIMWI katika michezo.

ix. Kuendeleza na kutambua vipaji vya vijana katika michezo kuanzia umri mdogo.

SEKTA YA MAENDELEO YA UTAMADUNI
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

SEKTA YA MAENDELEO YA SANAA
Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Jukwaani.
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

SEKTA YA MAENDELEO YA MICHEZO
Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news