NA DIRAMAKINI
UONGOZI wa Young Africans Sports Club (Yanga SC) ya jijini Dar es Salaam umesema umefikia makubaliano ya kuachana na Kocha wake, Nasreddine Nabi baada va kocha huyo kuomba kutoongeza mkataba mpya.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi huo kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano, Juni 14, 2023 ambapo imefafanua kuwa, “Mkataba wa Kocha Nasreddine Nabi na Klabu ya Young Africans Sports Club umemalizika mwisho wa msimu huu.
"Baada ya kumalizika kwa mkataba huo, uongozi wa Young Africans Sports Club ulikutana na Kocha Nabi kwa ajili ya mazungumzo ya kusaini mkataba mpya, lakini Nabi aliomba kuondoka ili akapate changamoto mpya.
“Akiwa Kocha Mkuu wa Young Africans Sports Club, Nabi amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya NBC, mataji mawili ya Kombe la Shirikisho la Azam, mataji mawili ya Ngao ya Jamii na kuifikisha Timu yetu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.
“Uongozi wa Young Africans Sports Club unamshukuru Kocha Nabi kwa mchango wake katika kipindi chote alichofanya kazi kwenye timu yetu na unamtakia kila la kheri katika safari yake, aidha Uongozi wa Young Africans Sports Club meanza mchakato wa kumpata Kocha mpya atakayechukua nafasi ya Kocha Nasreddine Nabi,”imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.