PWANI-Watu wawili wamefariki na watatu kujeruhiwa baada ya basi la abiria kugongana lori maeneo ya Tanita Kibaha mkoani Pwani.
Ajali hiyo imetokea Julai 26, 2023 saa 8:30 usiku, ikihusisha basi la Kampuni ya Saratoga lililokuwa likitokea mkoani Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam, ambapo liligongana lori la mafuta lilokuwa likitokea jijini humo kuelekea mikoani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Piusi Lutumo kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni kitendo cha dereva wa basi hilo, kutaka kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.
Pia, Kamanda huyo amemtaja mmoja wa waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo kuwa ni dereva wa basi hilo, Ammy Anuru mkazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam na abiria mwingine mwanaume ambaye jina lake halijafahamika.
Aidha,majeruhi wengine katika ajali hiyo ni Mnilu Mohamed mkazi wa Ujiji Mkoa wa Kigoma, Shabani Bomeka, mkazi wa Kigoma na Amani Jonathan mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam, ambao wote wanaendelea na matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Kamanda Lutumo amesema kuwa, miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani.(Mwananchi)