ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka waumini wa dini ya kiislamu nchini kuhubiri amani.
Wito huo ameutoa leo Julai 28,2023 wakati akihutubia baada ya sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Miembeni Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alhaj Rais Dkt. Mwinyi amesema, amani ndio msingi wa kila kitu, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa Zanzibar.
Pia, Rais Dkt. Mwinyi amehimiza umuhimu wa umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari ili kuendeleza na kujenga Zanzibar kimaendeleo.
"Umoja wetu ndio msingi wa kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar."