DAR ES SALAAM-Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila leo Julai 25, 2023 ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa huo kuadhimisha Siku ya Mashujaa katika viwanja vya Mashujaa Mnazimmoja jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila ameshiriki itifaki mbalimbali kuashiria maadhimisho hayo pia amewataka wananchi kuendelea kufanya matendo ya kizalendo na kishujaa kama walivyofanya wazee wetu ambao walipelekea ukombozi wa bara Afrika.
Aidha RC Chalamila amesema amani tunayoiona sasa haikupatika kwa urahisi, kwani wazee wetu walijitoa kwa hali na mali kulikomboa taifa hili, ndio hao ambao leo tuna wakumbuka kama mashujaa wa Taifa letu.
Vilevile, Mhe. Albert Chalamila amemshukuru Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuongoza harakati za kulikomboa taifa na viongozi wengine waliofuatia, lakini pia ametoa rai kwa jamii kuendelea kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo amekuwa akiliongoza Taifa hili vizuri, wananchi wanatekeleza majukumu yao ya kujiletea maendeleo kwa amani na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam,Adam Ngalawa ameitaka jamii kutumia kumbukizi hizi kuhamasishana uzalendo na kufanya matendo ya kishujaa kwa masilahi mapana ya Taifa letu.
Ifahamike kuwa maadhimisho hayo Dar es Salaam yameadhimishwa katika ngazi ya mkoa kitaifa yameadhimishwa Dodoma na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.