NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa Mikataba 3 ya msaada wa maendeleo inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) wenye thamani ya Euro milioni 179.35 sawa na Shilingi bilioni 455.09 za Kitanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini wa mikataba mitatu ya msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya yenye thamani ya Euro Milioni 179.35 sawa na Shilingi Bilioni 455.09 za Kitanzania na kupewa Msaada wa Bajeti ya Serikali kiasi cha Euro Milioni 46.11 sawa na Shilingi Bilioni 117.036 za Kitanzania kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 kutoka Umoja wa Ulaya. Mikataba hiyo imetiwa saini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt.Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Manfredo Fantl katika Ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma leo Julai 4, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kwenye Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba Mitatu ya Msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya yenye thamani ya Euro Milioni 179.35 sawa na Shilingi Bilioni 455.09 za Kitanzania na kupewa Msaada wa Bajeti ya Serikali kiasi cha Euro Milioni 46.11 sawa na Shilingi Bilioni 117.036 za Kitanzania kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 kutoka Umoja wa Ulaya. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hazina Mkoani Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya utiaji saini wa mikataba mitatu ya msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya yenye thamani ya Euro milioni 179.35 sawa na shilingi Bilioni 455.09 za Kitanzania na kupewa msaada wa Bajeti ya Serikali kiasi cha Euro Milioni 46.11 sawa na Shilingi Bilioni 117.036 za Kitanzania kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 kutoka Umoja wa Ulaya. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hazina Mkoani Dodoma leo Julai 4, 2023.
Aidha, Rais Samia ameshuhudia kutangazwa kwa fedha za msaada wa bajeti ya Serikali zilizotolewa na EU kiasi cha Euro milioni 46.11 sawa na Shilingi bilioni 117.036 za Kitanzania kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023.
Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta za maendeleo hasa katika uchumi wa Buluu, uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na uimarishaji mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa fedha serikalini.
Katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Hazina Rais Samia ameishukuru EU kwa
kuwa msaada huo ni matokeo ya ziara aliyoifanya Brussels, Ubelgiji alipokutana na
Rais wa Tume ya Ulaya Mhe. Ursula Von der Leyen.
Msaada huo uliotolewa kwa Serikali unaendana na mipango mkakati ya kisekta na maendeleo nchini, hususan Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Dira
ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050.
Aidha, Rais Samia amesema Programu hizo pia zitaendana na kaulimbiu ya Mwaka wa Fedha wa 2023/24, kama ilivyopitishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC):
"Kuongeza kasi ya kufufua uchumi, kukabiliana na kupunguza mabadiliko ya
tabianchi pamoja na kuimarisha sekta zenye tija kwa maisha bora".