DAR ES SALAAM-Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imetoa orodha ya wanufaika wa mirabaha ya Julai, 2023 kwa njia ya wanachama na kazi zilizosajiliwa.
Kwa mujibu wa orodha hiyo iliyotolewa na COSOTA,wanufaika wanaombwa kufika Ofisi ya COSOTA Majengo ya Utumishi,18 Barabara ya Kivukoni jijini Dar es Salaam kuanzia leo Julai 24,2023 saa 1:30 asubuhi hadi 09:30 jioni.
COSOTA, ipo chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na imeanzishwa chini ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki na 7 ya Mwaka 1999.
COSOTA ilianza rasmi mwaka 2001 ikiwa na majukumu makuu mawili, usimamizi wa hakimiliki nchini,lakini pia ukusanyaji na ugawaji mirabaha.
Kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2022 (Finance Act 2022) ilitenganisha majukumu hayo na kuanzisha makampuni binafsi ya kukusanya na kugawa mirabaha nchini (CMO),ambapo kwa sasa Ofisi ya Hakimiliki imebaki kusimamia masuala ya Hakimiliki na kutoa leseni kwa Makampuni yanayohusika na kukusanya na kugawa mirabaha (CMO) pamoja na kusimamia masuala ya uharamia wa kazi za wabunifu.