NA MWANDISHI WMJJWM
KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.John Jingu amekutana na kufanya Mazungumzo na Mwakilishi wa shirika la linalojishughulisha na masuala ya jinsia la NIRAS Tanzania, Dkt. Suma Kaare pamoja na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Guidet Chiara leo Julai 3, 2023 jijini Dodoma.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Sifuni Msangi.