NA MWANDISHI WETU
IMEELEZWA kuwa, Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu unaoendelea katika eneo la Magogo mkoani Geita unakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.
Hayo yameelezwa leo Julai 4, 2023 na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Geita Gold Mining Ltd, Doreen Dennis katika banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya 47 ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
"Uwanja wetu wa Magogo utakapo kamilika unakadiriwa kuchukua zaidi wa mashabiki elfu 20 kwa wakati mmoja ili kutazama mechi mbalimbali zitakazochezwa katika uwanja huo," amesema Doreen.

