Karibu Kiwanda cha nguo TAVEN Dodoma. Mkurugenzi Mtendaji wa Taven Industries Company Limited, Dkt.Gustavus Deusdedith amesema, nia ya kuanzisha kiwanda hiki ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa nguo za aina mbalimbali nchini ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Kiwanda hicho kilichopo Block D, Plot 716, Chihoni Kata ya Nala jijini Dodoma,licha ya kuunga mkono jitihada hizo kimetoa fursa za ajira kwa Watanzania mbalimbali.
Miongoni mwa huduma wanazotoa ni uzalishaji na usambazaji wa t-shirt (fulana) za aina zote zikiwemo za kola (polo),za round,zenye shingo v.
Pia, Kiwanda cha TAVEN kinatoa sare za aina zote za shule, za hoteli, viwanda na maeneo ya kazi, biashara na ulinzi. Nyingine ni nguo za mitindo mbalimbali kwani wanazalisha kwa mteja aliyeandaa mitindo au sampuli.
Unaweza kueta nguo ya sampuli au mchoro, nguo za watoto, nguo za safari, nguo za kutokea, nguo za kiofisi na sehemu rasmi na mitindo yote iliyoandaliwa au kuandaliwa na wataalamu wetu.
Mbali na hayo wanatoa huduma za uchapishaji wa nguo kwa njia ya kudarizi,kuchapa kwa njia ya wino na moto na michoro ya asili. Aidha, Kiwanda cha TAVEN Dodoma kinatoa ushauri na uelekezi.
JE? Unahitaji huduma yotote ya nguo zenye ubora wa hali ya juu, fanya uamuzi wa busara sasa, wasiliana na uongozi wa Kiwanda cha TAVEN kupitia simu 0716041476 au 0717514324 na 0715094290 utafurahia huduma za viwango vya hali ya juu;