Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Julai 3,2023


Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China umesema kumekuwa na matukio ya Watanzania wanaosafiri kwenda Hong Kong kuzuiliwa kuingia au kuhojiwa kwa muda mrefu na maafisa wa Idara ya Uhamiaji ya Hong Kong katika uwanja wa ndege wa Hong Kong, ambapo hali hiyo imejitokeza zaidi hivi karibuni tangu Hong Kong ifungue mipaka yake kuruhusu wageni baada ya miaka mitatu ya zuio la kuingia Hong Kong kwa ajili ya udhibiti wa UVIKO-19.

“Hatua hizo za Mamlaka za Hong Kong zimetokana na matukio ya siku za nyuma ambapo watu wachache waliokuwa na paspoti ya Tanzania kufanya vitendo vya uvunjivu wa sheria, Machi 30, 2023 Ubalozi umewasiliana na Mamlaka za Hong Kong kueleza kutoridhishwa na hatua hiyo inayochukuliwa na Maafisa wa Uhamiaji wa Hong Kong, Mamlaka za Hong Kong zilitujibu kwamba maafisa wao watatekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa mujibu wa sheria na wametoa rai kwa wasafiri wanaokwenda Hong Kong kuwa na nyaraka zote zinazohitajika.
















“Ubalozi unatoa rai kwa Watanzania wenye safari ya kwenda Hong Kong wahakikishe wana mwaliko kutoka kwa mwenyeji wa abiria ambaye anaweza kuwa mtu binafsi au kampuni, tiketi ya ndege yenye tarehe ya kuondoka Hong Kong, booking ya hoteli inayoonesha jina la msafiri, kuepuka kuvunja sheria za Hong Hong kwa kubeba vitu au bidhaa ambazo ni kinyume na sheria.

“Endapo Mtanzania yeyote atahitaji msaada au ufafanuzi zaidi awasiliane na Ubalozi kwa barua pepe: beijing@nje.go.tz au kwa simu kwa Afisa Ubalozi: +86 136 9336 0750 (Number hiyo haitumii whatsup- piga moja kwa moja).”











Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news