Jaji Mkuu wa Tanzania atoa pole

DAR ES SALAAM-Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma tarehe 24 Julai, 2023 ameitembelea familia aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kwa ajili ya kuipa pole kufuatia kifo cha mama yao mzazi, Bi. Elizabeth Augustine Saidi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimpa pole Bw. Daniel Saidi ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha mama yake mzazi, Bi. Elizabeth Augustine Saidi, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini tarehe 24 Julai, 2023 jijini Dar es Salaam.

Bi. Elizabeth Agustine Saidi alifariki dunia tarehe 21 Julai, 2023 jijini Dar es Salaam.Mhe. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma aliitembelea familia hiyo nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam na kuwapa pole ndugu ,jamaa na marafiki.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwapa pole wadogo wa mke wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha dada yao Bi. Elizabeth Augustine Saidi, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimpa pole Jenerali Mstaafu, Fara Mohamed ambaye ni mjomba wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha Bi. Elizabeth Augustine Saidi, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba huo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na familia ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha mama yao, Bi. Elizabeth Augustine Saidi.

Akizungumzia kuhusu msiba huo, mtoto wa marehemu, Bw. Daniel Saidi amesema misa na heshima za mwisho za kumwuaga mama yake zitafanyika siku ya Jumatano, tarehe 26, Julai2023 katika Kanisa la Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Petro (St. Peters), Osterbay, kuanzia saa 6 mchana hadi saa 9 alasiri . Kisha mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Marangu Moshi kwa mazishi.

Maziko ya mama Elizabeth Augustine Saidi yatafanyika siku ya Alahamisi tarehe 27 Julai, 2023 saa saba mchana nyumbani kwake Nduweni Marangu, Moshi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news