Kayombo akagua miradi ya elimu Kigoma Ujiji

KIGOMA-Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Vicent Kayombo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya elimu inayotekelezwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji mkoani Kigoma.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi huyo ameridhishwa namna miradi inavyotekelezwa huku akifanya vikao na walimu katika shule alizozitembelea na akisitiza suala la ufundishaji wenye matokeo mazuri ya ufaulu.

Aidha, katika ziara hiyo ametembelea Shule ya Sekondari Kigoma yenye ujenzi wa mabweni mawili, madarasa nane, na ujenzi wa matundu nane ya vyoo kwa gharama ya shilingi milioni 419 fedha kutoka Serikali Kuu.

Mradi mingine aliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa madarasa manne,ujenzi wa darasa moja la wanafunzi wenye mahitaji maalumu na ujenzi wa matundu matatu ya vyoo Shule ya Msingi Katubuka kwa gharama ya shilingi milioni 136.6.

Pia, ujenzi wa madarasa manne na ujenzi wa matundu manne ya vyoo Shule ya Msingi Kabingo kwa gharama ya shilingi milioni 112.800 kupitia mradi wa BOOST.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Bi. Mwantum Mgonja amempongeza Mkurugenzi wa Elimu-TAMISEMI kwa namna ambavyo ametembelea shule hizo na kutoa ushauri wa kitaaluma huku akiahidi kuendelea kusimamia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news