DAR ES SALAAM-Timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam (KMC FC) imeachana na wachezaji tisa.
Ni baada ya kumaliza mikataba yao na kusajili wengine nane kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwaka 2023/2024.
Matheo Antony, Nurdin Balora, David Kisu, Mohamed Samata, Frank Zakaria ,Issac Kachwele, Kelvin Kijili, Steve Nzigamasabo na Ally Ramadhan wamepewa asante.
Aidha,Wilbol Maseke, Rahimu Shomary, Fredy Tangalo, Vincent Abubakar, Andrew Simchimba, Juma Shemvuni, Rodges Gabriel na Twalib Mohamed wamepewa kandarasi mpya ndani ya timu hiyo.
KMC ambayo msimu ujao itakuwa chini ya kocha Mmarekani mzaliwa wa Somalia,Abdi Hamid Moallin inatarajiwa kuingia kambini jijini Zanzibar kwa maandalizi ya msimu wa 2023/24.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,Bi.Hanifa Suleiman Hamza na Mstaiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Songoro Mnyonge ndiyo waliongoza makabidhiano ya timu kwa kocha Abdi Hamid Moallin.
Tags
Dar es Salaam
Habari
Kinondoni
KMC FC
Ligi Kuu Tanzania Bara
Ligi Kuu ya NBC
Manispaa ya Kinondoni
Michezo
Usajili Ligi Kuu