KMKM kumenyana na St.George ya Ethiopia

MISRI-Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika timu ya KMKM imepangwa kucheza na timu ya St.George ya Ethiopia na mshindi wa mchezo huo atacheza dhidi ya bingwa mtetezi Al Ahly ya Misri.

Timu ya JKU ya Zanzibar ambayo inaiwakilisha Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika imepangwa kucheza dhidi ya Singida Fountain Gate ya Tanzania Bara na mshindi kati yao atakutana na Future Fc ya Misri katika mchezo wa kwanza kuelekea hatua ya makundi.

Aidha, Azam FC imepangwa kucheza dhidi ya Bahir Dar Kenema ya Ethiopia katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Afrika na mshindi wa jumla wa mchezo huo, atakutana na Club Africain ya Tunisia, kwenye raundi ya pili na atakayevuka hapo atatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Mshindi wa mechi kati ya Power Dynamos (Zambia) dhidi ya African Stars (Namibia) katika Ligi ya Mabingwa Afrika atakutana na Simba huku Yanga itaanzia Raundi ya Kwanza dhidi ya ASAS ya Djibouti, timu itakayoshinda itaingia Raundi ya Pili kuivaa Otoho ya Congo au Al Merrikh ya Sudan.

Droo hiyo ya CAF imepangwa Julai 25, 2023 na mechi hizo za awali zitachezwa kati ya Agosti 18, 19, na 20 huku mechi za marudiano ni kati ya Agosti 25, 26 na 27, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news