Maboresho ya bandari kushirikisha wadau

KIGOMA-Serikali imesema itaendelea kuhakikisha wadau wote wanashirikiswa katika hatua mbalimbali za maboresho ya bandari nchini ili kurahisisha shughuli za uchukuzi na kuongeza ufanisi wa bandari hizo.

Akizungumza mjini Kigoma wakati akifungua Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Maboresho ya Huduma za Bandari kwa bandari za Ziwa Tanganyika, Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Aron Kisaka amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha mizigo yote ya ndani na nje ya nchi hususani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inahudumia kupitia bandari ka Kigoma ili kurahisisha biashara.

“DRC pekee yake inatumia bandari ya Kigoma kwa kusafirisha zaidi ya tani elfu kumi sasa kwa maboresho tuliyoyafanya ndani ya kipindi hiki kifupi ni lazima tuhakikishe idadi ya mzigo unaohudumiwa unaongezeka ili thamani ya fedha iliyowekezwa ionekane,"amesema Mhandisi Kisaka.

Mhandisi Kisaka amesema pamoja na maboresho yanayoendelea kufanyika ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA kuhakikisha idara ya masoko inajipanga kutafuta mzigo kwa ajili ya bandari kubwa ya Karema ili kuifanya bandari hiyo kuwa na ufanisi baada ya ujenzi wake kukamilika.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Bw. Edward Mabula amesema zaidi ya shilingi bilioni 100 zimetumika kufanya maboresho ya miundombinu na vifaa katika bandari za Ziwa hilo ikiwemo bandari ya Kigoma, Kibirizi, Ujiji na Karema.

Bw. Mabula ameongeza kuwa kwa sasa TPA imeingia makubaliano na Serikali ya DRC kwa ajili ya kujenga bandari kavu eneo la Kalemi na Kasumbalesa ambapo hatua hiyo itaongeza usafirishaji wa shehena ya mizigo hadi kufikia tani laki 330.

Naye Mdau wa Bandari nchini na Mkurugenzi Mtendaji wa Malagarasi Shipping Company Bw. Mbarak Hamoud ameishukuru Serikali kwa kuanzisha vikao vya maboresho ya utendaji wa bandari kwani hatua hiyo itaongeza ufanisi na tija kwa kujadili na kutafuta suluhu kwa pamoja kwa hatua zote za maboresho yanayofanyika katika bandari hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news