NA MATHIAS CANAL
Bariadi-Simiyu
WAKAZI wa Kijiji cha Giriku Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai 2023 katika kata Bunamhala.
Uchaguzi huo utafanyika ili kukamilisha safu ya uongozi kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu Mheshimiwa Nhola Samora.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa kata hiyo uliofanyika katika vijiji tofauti tofauti, Mbunge wa Jimbo la Bariadi mkoani Simiyu, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew ameonya baadhi ya wanasiasa wanaowatishia wanachi watakaojitokeza kupiga kura.

"Anayezuia watu kumchagua kiongozi wao maana yake hataki maji, barabara, zahanati, umeme, kituo cha afya na dawa kwenye vituo cha afya."


Katika uchaguzi wa nafasi ya diwani katika kata ya Bunamhala jumla ya vyama 14 vinatarajiwa kushiriki kinyang'anyiro cha nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 13 Julai 2023.