RUVUMA-Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma wamehimizwa kuendelea kushirikiana katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kuhakikisha miradi ya maendeleo inafanikiwa na kutoa huduma sawa sawa kwa wananchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,Mhe. Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho akikabidhi pikipiki watendaji wa kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Peramiho.
Hayo yamesemwa Julai 6, 2023 mkoani Ruvuma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pikipiki tisa kwa watendaji wa kata wa Chama Cha Mapinduzi.
Watendaji wa kata zilizokabidhiwa pikipiki hizo ni Kata ya Peramiho, Maposeni, Ndogosi, Kilagano, Parangu, Kizuka, Litapwasi, Muhukuru na Mpandangindo.

“Vifaa hivi visaidie kukibeba chama kwanza, katika kusaidia kuongeza idadi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika maeneo yetu.”
Ameongeza kuwa, Jimbo la Peramiho ni miongoni mwa majimbo yanayofanya vizuri katika shughuli za serikali na shughuli za chama.
Pia amesema, Halmashauri ya Songea imepata hati safi mara mbili mfululizo, "hiyo ni ishara kwamba uongozi wa chama na uongozi wa serikali wametambua wajibu wao,"alisema Waziri Mhagama.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Songea Vijijini ametoa rai kwa watendaji wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuimarisha uwajibikaji na kumarisha mahusiano yao ya kiutendaji.
“Tuendelee kuwaimarisha na kuwasimamia waheshimiwa madiwani, kila mmoja kwenye eneo lake.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea, Mhe. Menas Komba amesema, watendaji wa chama wanapaswa kuhakikisha kura za chama zinapatikana kiutendaji kwa kuhakikisha mikutano inafanyika katika ngazi ya mabalozi na ngazi ya vitongoji.
Awali Katibu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Songea Vijijini, Juma Nambaila alisema, moja ya eneo ambalo watalisimamia kikamilifu ni kuwapima makatibu wa kata kwa uwajibikaji wao wa shughuli za chama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama na Mbunge wa Peramiho akiwa katika picha ya pamoja na watendaji kata wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Peramiho wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pikipiki.
Akitoa shukrani Diwani wa Kata ya Kizuka, Mhe.Jackob Nditi amesema, watatunza vitendea kazi na kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa chama kutekeleza maelekezo yanayotolewa na viongozi.