Mheshimiwa Mhagama awakumbusha jambo wawekezaji jimboni

RUVUMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho ametoa rai kwa wawekezaji wa mbalimbali katika Jimbo la Peramiho kuendelea Kufanya uwekezaji wenye tija kwa wananchi, kwa Halmashauri na kwa Taifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe.Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nakawale alipotembelea kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo ameyasema Julai 12, 2023 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Muhukuru katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Songea mkoani Ruvuma.

“Tunataka wawekezaji wajue wana wajibu wa kuchangia shughuli za maendeleo kwenye vijiji vinavozunguka maeneo ya uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe.Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho akizungumza na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Songea Vijijini,Thomas Masolwa (kushoto) wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Nakawale.

"Makaa ya mawe yamekuwa bidhaa muhimu na adhimu, uwekezaji umeendelea kukua na masoko yameongezeka, wawekezaji waangalie ajira zile zinazosaidia kuendesha miradi yao ili kutoa kipaombele katika maeneo ya vijjiji vilivyozunguka mradi.

“Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya kazi nzuri ya kuvutia wawekezaji mbalimbali, wawekezaji wa shamba la miwa,wawekezaji wa makaa ya mawe, na wawekezaji wa umeme wa maji, naomba kila mwekezaji aliyeomba ardhi ya uwekezaji atumie kama alivyoomba,”alibainisha Waziri Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho akizungumza na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea,Mheshimiwa Menas Komba (kulia) wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Nakawale.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mhe.Menas Komba amesema, uwekezaji wa makaa ya mawe kuna mpango kabambe ambao umelenga kupata asilimia moja ya kila awamu ya mauzo.

“Tuendele kushirikiana na wawekezaji wanaokuja kuwekeza ili waendelee kutusaidia na halmashauri itasimamia kupata haki za wananchi,”alisema Mhe.Komba.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mwalimu Neema Maghembe amesema, wawekezaji wote waliowekeza katika Halmashauri ya Songea wamefuata taratibu zote za uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe.Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nakawale, Abdalah Shaibu (kulia) wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Nakawale. 

“Tunawawekezaji wa kutosha, wengine wanaendelea na kazi za tafiti mbalimbali na wengine wako katika hatua ya kuanza uchimbaji wa makaa ya mawe,”alisema Mwalimu Maghembe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news