NA VERONICA MWAFISI
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa umma kuleta tija katika utendaji kazi wao ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 22 Aprili, 2023 kwa mara ya kwanza ambapo alielekeza kuwa, anataka utumishi wa umma wenye tija kwa kila mtumishi ili kutoa huduma bora kwa mendeleo kwa Taifa.
Mhe. Kikwete amesema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoani Pwani akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi wa umma mkoani humo.
“Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alieleza wazi kuwa halmashauri zake, watendaji na watumishi wote ni lazima wawe na tija katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuleta maendeleo nchini,” amesema Mhe. Kikwete.
Sehemu ya watumishi wa Mkoa wa Pwani na Halmashauri ya Mji wa Kibaha wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Vile vile, Mhe. Kikwete amewataka watumishi hao kubadilika ili kuendana na matakwa ya Serikali ya Awamu ya Sita ikiwemo uaminifu katika utekelezaji wa miradi mbambali ya maendeleo nchini na kwa kuzingatia ubora.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon akitoa utambulisho wa viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha kabla ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuzungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili katika halmashauri hiyo.
Aidha, Mhe. Kikwete amesema kuwa, mafanikio ya taasisi au taifa lolote yanategemea aina ya watumishi wanaoitumikia Serikali yao wakati wa utekelezaji wa majukumu ambapo wakitekeleza kwa weledi na ufanisi mkubwa yataleta chachu kwa maendeleo ya nchi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Kikwete iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili katika halmashauri hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mji Kibaha, Mhandisi Mshamu Munde amemshukuru Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kufanya ziara katika mkoa huo na kuahidi kuwa yeye pamoja na watumishi wenzake watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwani kwa kutokufanya hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu.
Katibu Tawala, Mkoa wa Pwani, Bw. Rashid Mchata akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wa Pwani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo.
Mkurugenzi wa Mji Kibaha, Mhandisi Mshamu Munde akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuhitimisha kikao kazi na watumishi wa Mkoa wa Pwani na Halmashauri ya Mji Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili.
Mtumishi wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Bw. Issa Hasani (Aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo Mkoa wa Pwani iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF katika mkoa huo.