NAIROBI-Pambano la marudiano lililowakutanisha bondia Mtanzania Karim Mandonga (Mtu Kazi) dhidi ya Mkenya Daniel Wanyonyi limemalizika kwa Mandonga kuchapwa.
Pambano hilo la uzani wa Light heavyweight lililoandaliwa katika Kituo cha Maonyesho cha Sarit jijini Nairobi lilifanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili ya Julai 23, 2023.
Licha ya kuwa ugenini, Mandonga bado alikuwa na idadi kubwa ya mashabiki ambao walimshangilia kwa kwa sauti ya juu, wakimtia moyo kumtandika Wanyonyi.
Majaji watatu walimpa Wanyonyi ushindi. Jaji George Athmani alimpa Wanyonyi alama 100-80, Jaji Wycliffe Marende 100-80, na Jaji Leonard Wanga 100-89.
Hili ni Pambano la pili kwa mabondia hao wa Afrika Mashariki kukutana, pambano la kwanza lililofanyika Januari 2023 huko huko Nairobi, Mandonga alimchapa Wanyonyi. (BBC).

Miimi ni Mkenya naa tunampenda sana Mandonga. Akiretire boxing anaweza kuwa mtangazaji mzuri sana wa michezo hapa Kenya. Yuko pia na hicho kipawa
ReplyDelete