NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Mhe.Balozi Dkt.Batilda Buriani ametembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) ambapo alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi.Latifa Khamis ambaye alimuongoza katika kutembelea mabanda mbalimbali ikiwa ni pamoja na Banda la Bidhaa za Asali.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Balozi Dkt. Batilda amepongeza bidhaa zilizooneshwa katika banda la asali na kusema kuwa ni za viwango vya juu na nyingi zinazalishwa katika Mkoa wa Tabora.

Pia akiwa katika Banda la Shirika Umeme Tanzania (TANESCO), Mhe. Balozi Dkt.Batilda amejionea miradi ya kimkati inayofanywa na shirika hilo kwa teknolojia ya Visual Reality.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi. Latifa Khamis amefurahiswa na jinsi ambavyo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeweka teknolojia ya Visual Reality ambayo inamuwezesha mtembeleaji wa banda hilo kuona picha halisi za miradi ya kimkakati unayotekelezwa na shirika hilo.