Mtumishi wa Umma ameza hongo aliyochukua baada ya kuona timu ya Kikosi Maalum cha Polisi

NA DIRAMAKINI

AFISA wa Serikali anayetunza kumbukumbu za umiliki wa ardhi (Patwari) katika Idara ya Mapato huko Katni Wilaya ya Madhya Pradesh nchini India anadaiwa kumeza fedha alizochukua kama hongo baada ya kuona timu ya Kikosi Maalum cha Polisi cha Lokayukta (SPE).

Vyombo mbalimbali vya habari nchini humo vimeripoti kuwa, tukio hilo limetokea leo Julai 25, 2023 wilayani Madhya Pradesh.

Kisa hicho kilitokea wakati afisa huyo aliyetambulika kwa jina la Gajendra Singh akipokea sehemu ya Rupia 5000 (zaidi ya shilingi 149,685 za Kitanzania) kama hongo katika ofisi yake binafsi iliyopo Bilhari wilayani humo kama sehemu ya mtego, Msimamizi wa Polisi wa SPE Sanjay Sahu alisema.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, Gajendra Singh alishawishi kupatiwa hongo hiyo kutoka kwa Chandan Singh Lodhi mkazi wa Barkheda wilayani humo kwa ajili ya kumuwezesha kuwekewa mipaka katika ardhi yake. Baada ya afisa huyo kutaka kiasi hicho cha fedha, Lodhi alikwenda kutoa taarifa Lokayukta Police Jabalpur.

“Mwanaume kutoka Kijiji cha Barkheda alikuwa ametulalamikia akidai Singh alikuwa akitafuta hongo. Baada ya kupokea fedha hizo, patwari aliona timu ya SPE na kumeza fedha. Alikimbizwa katika hospitali ambapo madaktari walisema alikuwa mzima,”afisa huyo alisema.

Mkaguzi wa Lokayukta Kamal Kant Uikey alisema, "malalamiko ambayo Lodhi alituma maombi ya kuwekewa mipaka ya ardhi ya babu yake Puranlal na uwekaji mipaka ulifanyika mnamo Julai 5,2023.

"Patwani, Gajendra Singh anayehusika alikuwa akidai hongo ya Rupia 5000 badala ya kuweka mipaka hiyo. Baada ya hapo mpango huo ulikamilika kwa Rupia 4500 (zaidi ya shilingi za Kitanzania 134,717."

Hata hivyo, kwa mujibu wa Jeshi la Polisi wilayani humo, kesi imesajiliwa dhidi yake na uchunguzi zaidi ulikuwa ukiendelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news