Naibu Waziri Nderiananga amshukuru Rais Dkt.Samia

NA MATHIAS CANAL
Kilimanjaro

MBUNGE wa Viti Maalumu, Mheshimiwa Ummy Nderiananga ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) akiwa katika ziara mkoani Kilimanjaro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa imani kubwa aliyompatia ya kumteua kuwa Naibu Waziri.
Akizungumza Katika mkutano na wananchi uliofanyika katika kijijini kwao Lotima ambapo ndipo alipozaliwa katika Kata ya Makuyuni ambapo ameeleza umuhimu wa shule za kata katika kuimarisha elimu nchini kwani zimeongeza chachu ya mafanikio kwa wananchi ambapo ametolea mfano yeye ambaye alisoma katika shule hizo.

Amesema kuwa, Rais anafanya kazi usiku na mchana hivyo watanzania wanapaswa kumtia moyo na kumuunga mkono ili aweze kufikia dhamira ya kuwaletea maendeleo endelevu.
"Mhe Rais Samia ana upendo mkubwa na wana Kilimanjaro na sisi wanamakuyuni tumeona upendo wake, tumeona kujali kwake na kuthamini kwake,"amesema Nderiananga.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Vunjo,Mheshimiwa Dkt.Charles Kimei amemshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuendelea kuboresha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo utengenezaji wa barabara ya Himo-Makuyuni kwa kiwango cha lami ambayo imeshaanza kutengenezwa.

Amesema kuwa, ujenzi wa barabara hiyo utarahisisha huduma za kijamii ikiwemo usafirishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mheshimiwa Kisare Makori ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa miradi mingi ya maendeleo katika Wilaya ya Moshi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news