ARUSHA-Paroko wa Kanisa la Katoliki, Parokia ya Karatu mkoani Arusha, Pamphili Nada ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito.
Tukio hilo linadaiwa kutendwa na mtu anayedaiwa kuwa na tatizo la afya ya akili aliyeingia kanisani kwa nguvu kutaka kusali.
Mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Romani Leonard (30) baada ya kufanya mauaji hayo naye ameuawa na wananchi wenye hasira.
Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo leo Julai 19, 2023.
"Padri alifariki wakati anapelekwa hospitali na mtuhumiwa aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kupata taarifa za tukio hilo,"amesema.