Polisi yapiga marufuku maandamano ya UVCCM

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi nchini limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) katika wilaya zote nchini kwa kusema kuwa, kuitisha maandamano nchi nzima kwa lengo la kuiunga mkono Serikali juu ya uwekezaji katika bandari ni sawa na kuleta vurugu na hofu kwa Watanzania.

Aidha, jeshi hilo limewataka wote wenye nia kama hiyo wawasilishe hoja zao kupitia mikutano na vyombo vya habari.

Awali, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa,Mohammed Ali Kawaida akizungumza na waandishi wa habari alisema, umoja huo unaunga mkono uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Kupitia mkutano huo uliofanyika kwenye ofisi ndogo za Makao Makuu ya UVCCM Upanga jijini Dar es Salaam, Kawaida alisisitiza kuwepo kwa maandamano ya amani ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuboresha, kuendesha na kuendeleza maeneo ya bandari nchini.

Aidha, Kawaida alisema maandamano hayo yatafanyika nchi nzima ambapo yatazinduliwa rasmi mkoani Dar es Salaam siku ya tarehe 18 Julai, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news