RIYADH/NIAMEY-Serikali ya Ufalme wa Saudi Arabia imetoa wito wa kuachiliwa huru mara moja kwa Rais wa Jamhuri ya Niger, Mohamed Bazoum.
Kanali Meja Amadou Adramane akitangaza mapinduzi hayo kupitia runinga ya Taifa. (Picha na Skynews).
Bazoum aliondolewa madarakani siku ya Jumatano, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa kundi la wanajeshi walioonekana kwenye televisheni ya taifa hilo la Afrika Magharibi saa chache baada ya rais kushikiliwa katika ikulu ya rais.
Katika taarifa ya pili kuhusu hali ya kisiasa nchini Niger, Saudi Arabia ilieleza kukataa kabisa jaribio la kupindua uhalali wa Rais Bazoum.
"Tunatoa wito kwa muungano wa wanamapinduzi kumwachilia haraka rais na kumwezesha kurejeshewa moja kwa moja mamlaka yake ya kikatiba huku akihakikishiwa usalama na ustawi wake," Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia ilieleza kama ilivyonukuliwa na SG.
Pia, wizara ilirejea wito wa Ufalme wa kutoa kipaumbele kwa maslahi ya Niger na watu wake ili kuepuka machafuko ya kisiasa ambayo yanaweza kuweka maisha na rasilimali za taifa hilo katika hatari.
Awali, Shirika la Habari la Reuters liliripoti kuwa,walinzi wa Rais Mohamed Bazoum walimshikilia ndani ya Ikulu iliyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Niamey.
Hayo yalikuwa ni kwa mujibu wa vyanzo vya usalama ingawa ofisi ya rais ilisema walinzi walianzisha vuguvugu dhidi ya jamhuri bila mafanikio na kwamba Bazoum yuko salama.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imesema, ina wasiwasi kuhusu jaribio la mapinduzi na kuwataka waliopanga njama kumuachia huru Rais Bazoum.
Jeshi la taifa lilikuwa tayari kuwashambulia walinzi hao endapo hawatajirudi, ilisema taarifa kutoka ofisi ya rais. Taarifa hiyo ilifuatia ripoti kuwa walinzi wa rais wamekata mawasiliano ya kuingia Ikulu na kumzuia rais Bazoum akiwa ndani, kuongeza wasiwasi wa kutokea kwa mapinduzi ya sita katika nchi za Afrika Magharibi tangu 2020.
"Rais wa Jamhuri na familia yake wako salama," ofisi ya rais ilisema kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii bila kutoa maelezo zaidi.
Taarifa hiyo ilifutwa baadaye huku kukiwa na mashaka juu ya nani alikuwa anadhibiti. Wanajeshi walikuwa wamechukua udhibiti wa barabara zote zinazoelekea kwenye kituo cha taifa cha televisheni ambacho kilikuwa kikionesha sinema.
Aidha, maeneo mengine ya mji wa Niamey yalikuwa shwari, magari barabarani yalikuwa kama kawaida na huduma za intaneti zilikuwa nzuri, mwandishi wa habari wa Reuters alisema.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa ECOWAS ambaye ni Rais wa Nigeria, Bola Tinubu amesema, jumuiya hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa demokrasia inadumishwa nchini Niger.
Wakati huo huo, Serikali ya Ufaransa kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Catherine Colonna imelaani kwa nguvu zote hatua hiyo ya jeshi na kutoa wito kwa ECOWAS na AU kurejesha demokrasia nchini Niger.
Marekani ambayo ni mshirika wa karibu wa Niger, nayo imelaani hatua hiyo na Waziri wake wa Mambo ya Nje,Anthony Blinken amesema, wanafuatilia kwa karibu hali hiyo.
‘‘Tunafuatilia kwa karibu matukio nchini Niger, nilizungumza na Rais Bazuom na kumhakikishia kwamba Marekani inamuunga mkono kama rais aliyechaguliwa kihalali kule Niger,’’amesema Blinken.
Mohamed Bazoum mwenye umri wa miaka 63 ni mwanasiasa wa Niger ambaye ni rais wa sasa wa Jamhuri ya Niger. Amekuwa ofisini tangu Aprili 2, 2021 baada ya kushinda Uchaguzi wa Urais 2020-2021.
Kabla ya kuwa Rais, aliwahi kuwa Rais wa Chama cha Demokrasia na Ujamaa cha Niger (Nigerien Party for Democracy and Socialism).
Uchaguzi mkuu ulifanyika nchini Niger tarehe 27 Desemba 2020 ili kumchagua Rais na Bunge la Kitaifa. Kwa vile hakuna mgombea wa urais aliyepata kura nyingi, duru ya pili ilifanyika tarehe 21 Februari 2021.
Mohamed Bazoum alitangazwa mshindi katika duru ya pili kwa kupata asilimia 55.67 ya kura huku nafasi ya pili ikichukuliwa kwa asilimia 44.33 na Mahamane Ousmane.
Rais aliyemaliza muda wake Mahamadou Issoufou alimaliza muhula wake wa pili mwaka 2021 na kutangaza hadharani kung'atuka, na hivyo kufungua njia ya mpito wa kwanza wa madaraka kwa amani nchini humo tangu uhuru.
Rekodi ya idadi ya wagombea 41 waliomba kugombea urais, lakini 30 pekee ndiyo walikubaliwa. Miongoni mwa wagombea 11 waliokataliwa ni Hama Amadou, mgombea wa chama kikuu cha upinzani, ambaye maombi yake yalikataliwa na mahakama ya kikatiba kutokana na kifungo chake cha awali kwa mwaka mmoja katika kesi ya ulanguzi wa watoto.
Amadou, ambaye aliibuka wa pili katika uchaguzi wa 2016 na wa tatu katika uchaguzi wa 2011, alikanusha mashtaka yote na kudai kuwa yalichochewa kisiasa.