ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezitaka taasisi za Serikali na jumuiya zote za waajiri na waajiriwa wahakikishe wanawasilisha michango katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa wakati ili kurahisisha shughuli za uendeshaji wa mfuko huo katika kuwajengea misingi mizuri wafanyakazi wao wanapostaafu na kuhitaji mafao yao.

Rais Dkt.Mwinyi amewashauri wajasiriamali wote wajisajili na kuchangia Mfuko wa Hiari kupitia mfuko huo, kwani una faida kubwa kwa biashara zao.
Vilevile, amewapongeza ZSSF kwa kuanza kulipa mafao mapya mawili kwa wanachama wake waliopoteza ajira na walioumia wakiwa kazini.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza ZSSF kwa kuzingatia utekelezaji wa agizo lake alilolitoa Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi mwaka huu (2023) kuongezeka kwa malipo ya pensheni kwa wastaafu.