Rais Dkt.Samia amerejesha tabasamu kupitia TASAF

NA VERONICA MWAFISI

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza nia yake ya dhati katika kuwafikia Watanzania wenye mahitaji kupitia mradi wa TASAF ili kuwanusuru wananchi walio na hali duni ya maisha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitazama baadhi ya bidhaa za walengwa wa TASAF zinazouzwa katika Mtaa wa Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Kibaha.

Mhe. Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akimtambulisha Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Bw. Henry Mbago (kushoto) kwa wananchi na walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Kibaha.

Mhe. Kikwete amesema kuwa, katika utekelezaji wa majukumu ya Rais Mhe. Dkt. Samia ndani ya miaka miwili ya uongozi wake zaidi ya Shilingi bilioni hamsini na moja zimeweza kutumika ili kuwasaidia wananchi wenye hali duni ambao wanakidhi kunufaika na mradi wa TASAF.
Baadhi ya wananchi na walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza na wananchi na walengwa hao wa TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Kibaha.

Mhe. Kikwete amewataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyedhihirisha nia yake ya dhati kwa vitendo katika kuwainua kimaisha Watanzania wenye hali duni kupitia mradi wa TASAF.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon amewapongeza walengwa wa TASAF, wanaofanya biashara kupitia mikopo mbalimbali wanayoipata kutokana na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Naye, mlengwa wa TASAF, Bi. Mariam Pazzi amesema kwa niaba ya walengwa wenzake wa TASAF wanamshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia kwa kuwawezesha kupata mikopo mbalimbali ambayo imewawezesha kufanya biashara kupitia vikundi mbalimbali hivyo kuwawezesha kuinuka kimaisha.
Mlengwa wa TASAF, Bi. Mariam Pazzi akitoa shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kufanya ziara katika Mtaa wa Miwaleni, Tarafa ya Kongowe, Wilaya ya Kibaha kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Mji Kibaha.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete yupo katika ziara ya kikazi ya wiki moja katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao pamoja na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news