Rais Dkt.Samia atoa tamko

DODOMA-Anaandika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, "Leo nchi yetu inaadhimisha siku adhimu kuwakumbuka mashujaa wetu. 
Hii ni miamba na majabali ya kihistoria ambayo kwa kujitoa kwao kwa hali na mali kumetufanya sisi kuwa huru, kuishi huru, kuwa na Taifa letu, nyumbani kwetu, na kuwa hapa tulipo kama nchi. 

Tunajenga mnara mrefu zaidi barani Afrika katika Jiji la Dodoma kama sehemu ya kuendelea kuwaenzi mashujaa wetu. 
Mnara huu ni alama nyingine ya uhuru wetu, shukrani yetu na kujitambua kwetu wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunakwenda. 

Nawaelekeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na wote wanaohusika na ujenzi huu wa kihistoria kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango. 
Siku hii pia ni siku ya tafakari. Tafakari ya kuendelea kuyaishi waliyoyaamini na kuyasimamia mashujaa wetu kwa kutunza amani, umoja, utulivu, mshikamano na kufanya kazi kwa bidii kwa Taifa letu. 
Katika siku hii muhimu, tuendelee pia kukumbuka na kuzingatia kuwa Tanzania ni moja, itabaki kuwa moja na kamwe haitagawanyika. Tusikubali na hatutaruhusu mtu yeyote au kikundi chochote kutugawa kwa kisingizio chochote kile." 

Mwenyezi Mungu Ibariki Afrika. 
Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news