NA LWAGA MWAMBANDE
NENO la Mungu kupitia Biblia Takatifu, rejea Isaya 38:1-2 inafafanua kuwa, 1; Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana (Mungu) asema hivi,tengeneza mambo ya nyumba yako, maana utakufa, wala hutapona.
Ukiendelea mstari wa 2; unaendelea kufafanua kuwa,basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamuomba Bwana.
Ukitafakari neno la Mungu kwa kina utaona namna ambavyo kuna umuhimu wa kutengeneza mambo ya nyumba yako, ndiyo maana neno linaanza na kutuambia siku hizo Hezekia aliugua.
Ni wazi, tunafahamu mtu akiugua anakuwa dhaifu, hana nguvu sawa sawa, muda mwingine kuugua kunaweza kumpelekea mtu kukata tamaa sasa kule kukata tamaa kunampelekea mtu kufa kabisa.
Aidha, neno linazidi kusema Hezekia alikuwa katika hali ya kufa, maana yake saa yoyote, muda wowote Mfalme Hezekia angekufa, ashukuriwe Mungu, muumba Mbingu na Nchi alimtuma Nabii Isaya kwenda kwa Mfalme Hezekia kumpa taarifa ya matengenezo.
Pia, rejea Biblia Takatifu kitabu cha 2 Wafalme 20:12-19 utaona namna ambavyo shetani anapambana kumtoa mtu kwenye mpango wa Mungu. Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasisitiza kuwa,kupitia Mfalme Hezekia tuna jambo la kujifunza. Endelea;

1.Kiburi cha Hezekia, kitu tunajifunzia,
Ili tusijerudia, sote tukaangamia,
Huyu twamkumbukia, magumu alipitia,
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
2.Alipigwa Hezekia, ugonjwa wa kuishia,
Nabii akamjia, ya Mungu kumpatia,
Ya kwamba atajifia, aweze jiandalia,
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
3.Kusikia Hezekia, kwamba kifo chamjia,
Mungu akamlilia, aweze mhurumia,
Mungu akamsikia, kifo mbatilishia,
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
4.Miaka kampatia, kumi na tano sikia,
Afya ikamrudia, maisha kufurahia,
Mabaya kamfanyia, hadi Mungu kachukia,
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
5.Ujinga lijifanyia, siri kujitangazia,
Ujumbe kuuambia, siri wakachungulia,
Fahari lifikiria, kumbe anaangamia,
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
6:Nabii akamjia, ghadhabu kumshushia,
Mabaya tamfikia, yeye akiashaishia,
Lifurahi Hezekia, yeye kijiangalia,
6.Watoto kufikiria, utowashi kuishia,
Mali alojichumia, kwamba zitachikichia,
Hilo hakufikiria, yake alijijalia,
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
7.Utumwa kuwaingia, afurahi Hezekia,
Watavyowafanyizia, wala hakuangalia,
Yake kuyaangalia, ndiyo alikazania
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
8.Badala ya kutubia, yale alijifanyia,
Mungu aweze sikia, rehema kuwapatia,
Yeye alifurahia, kwa amani taishia,
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
9.Mungu hivyo achukia, hapendi akasikia,
Somo hilo angalia, yote unajifanyia,
Kwake ukijafikia, hukumu itakujia,
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
10.Mali unajipatia, nguvu zako waringia,
Yale unajifanyia, mara mbili fikiria,
Kesho itapoingia, nao watafurahia?
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
11.Tukuite Hezekia, asali wajilambia,
Rungu likiwashukia, wewe hautasikia?
Ndugu yangu angalia, hukumu yakukalia,
Tusijipende wenyewe, tutelekeze kizazi.
12.Wewe umetangulia, wako wanaofwatia,
Hati umeshikilia, vema ukiwapatia,
Chini sijewabwagia, wawe wa kuangamia,
Tusijipende wenyewe tutelekeze kizazi.
13.Sisi kina Hezekia, hekima twahitajia,
Tuweze kusimamia, mali uzotupatia,
Wajukuu kiingia, wakawaweze furahia,
Tusijepende wenyewe, tutelekeze kizazi.
(2 Wafalme 20: 12-19)
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602