DAR ES SALAAM-Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw.Saidi Yakubu amesema, Serikali imepanga kujenga viwanja viwili vya michjezo nchini katika mkoa wa Arusha na Dodoma ili vitumike katika michuano ya Kombe la Afrika mwaka 2027 vyenye uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 kila kimoja.

Aidha, Serikali imejipanga kuboresha na kukarabati viwanja saba vya Uhuru, Uwanja wa Benjamin Mkapa vya Dar es Salaam, Uwanja wa Sheikh Abeid Arusha, Uwanja wa Sokoine Mbeya, Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na Mkwakwani Tanga.
Amesema, pia Serikali inajenga pia viwanja vya wananchi kupumzikia katika jiji la Dar es Salaam na Dodoma pamoja na Arena mbili katika mikoa hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CREC, Bw. He Yeting kutoka nchini China amesema, wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika eneo la kuboresha miundombinu ya michezo hapa nchini kuilingana na mahitaji ya wakati huu.