Serikali kutoa fungu ujenzi wa Kituo cha Afya Peramiho

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amesema, Waziri Mhe.Angellah Kairuki ameahidi kuwa Serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Peramiho ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango aliyoyatoa mara baada ya Mbunge wa Peramiho, Mhe.Jenista Mhagama kuwasilisha ombi la kujengewa kituo cha afya.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wa Peramiho (hawapo pichani), mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango kumpatia fursa ya kuzungumza na wanachi wa eneo hilo. 

Mhe. Ndejembi ametoa ahadi hiyo kwa wananchi wa Peramiho kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki, mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango kumpatia fursa ya kuzungumza na wananchi hao.

Mhe. Ndejembi amesema kwa heshima na maelekezo ya Makamu wa Rais, fedha hiyo itatolewa mapema iwezekanavyo ili kuwezesha ujenzi wa kituo cha afya ambacho kitaboresha utoaji wa huduma za afya kwa jamii.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango akikata utepe kuzindua kituo cha afya Lilambo mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho kilichojengwa katika Kijiji cha Kigonsera. 

“Ujenzi wa kituo hicho unatokana na jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Peramiho Mhe. Jenista Mhagama ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni ataleta gari mbili za kubebea wagonjwa katika Halmashuri ya Wilaya ya Songea, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa maboresho ya utoaji wa huduma za afya katika Hamashauri hiyo.
Wananchi wa Peramiho wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango kumpatia fursa ya kuzungumza nao.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesema kuwa mafanikio ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wilayani Songea na katika maeneo mengine yanajianisha wazi kupitia kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya elimu ya awali, msingi na sekondari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news