Serikali kutoa kipaumbele ajira huduma za utengamao

DAR ES SALAAM-Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu amesema, Serikali itatoa kipaumbele cha ajira kwa wataalam wa huduma za utengamao (Rehabilitative Services) kupitia watu waliosomea fani za Physiotherapy, Occupationa Therapy, pamoja na Audiology and Speech Language.

Waziri Ummy amesema hayo mara baada ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kutoa tangazo la fursa za masomo kwa fani hizo.

“Tuna uhaba wa wataalam hawa katika nchi yetu, hakika uwepo wao unakwenda kuwezesha watu wenye ulemavu hususani watoto kuishi maisha bora zaidi,”amesema Waziri Ummy.

Amesema kuwa, amefurahi kuona kozi za shahada ya kwanza za wataalamu wa Huduma za Utengamao na kukipongeza Chuo cha Muhimbili kuja na kozi hizo muhimu katika Sekta ya Afya.

"Niwatie moyo wenye sifa za kusoma kozi hii kuomba. Serikali kupitia Wizara ya Afya itatoa kipaumbele cha ajira kwa wataalam hawa,"amesema Waziri Ummy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news