NA GODFREY NNKO
KAMISHNA wa Kinga na Huduma za Utengamao wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Bi.Moza Makumbuli amebainisha kuwa, Tanzania inaongoza kuwa na sheria kali kwenye udhibiti wa dawa za kulevya.
Hayo ameyabainisha kupitia mahojiano na kipindi cha Ndingani cha East Africa Redio ya jijini Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi kuhusu Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2015 juu ya makosa na adhabu.
"Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2015 kwa kweli ni kali sana, ukiangalia tu kwa mfano dawa hizi za unga kama Cocaine au Heroin ukikutwa na gramu kuanzia 201 mwisho unaweza kukutwa na kifungo hadi cha miaka 30.
"Lakini ikivuka mia mbili na moja na kuendelea kifungo cha maisha kinakuhusu, ndiyo sheria yetu inavyosema hivyo, lakini hizi bangi kwa kweli ukikutwa na kilo zaidi ya 20 ni kifungo kisichozidi miaka 30.
"Na ikivuka kilo 100 na kitu, kifungo cha maisha kinakuhusu kwa hiyo tunaweza kusema katika hizi nchi za Afrika Mashariki na Kati, Tanzania ni moja kati ya nchi ambayo ina sheria kali sana ukikutwa dawa za kulevya.
"Kuna watu ambao wamehukumiwa katika baadhi ya mikoa, watu wanashangaa yaani bangi tu mtu anafungwa kifungo cha maisha au kukutwa na mirungi?Ndiyo, kwa sababu sheria yetu ni kali sana.,"amefafanua Kamishna Makumbuli.
Kuhusu DCEA
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ilianzishwa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya Mwaka 2015. Sheria hii iliifuta Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya. Kuanzishwa kwa Mamlaka Kulitokana na mapungufu yaliyokuwepo katika mfumo wa udhibiti wa dawa za kulevya.
Mapungufu hayo yalikuwa ni pamoja na Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya iliyoanzishwa na Sheria ya ya Kuzuia Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya Namba 9 ya mwaka 1995 kukosa nguvu ya kisheria ya kupeleleza, kufanya uchunguzi na kukamata wahalifu wa dawa za kulevya.
Kutokana na mapungufu hayo, Baraza la Mawaziri katika kikao chake cha tarehe 8 Novemba, 2007 (Waraka Na 60/2007) liliagiza, kurekebisha au kufuta Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya Namba 9 ya mwaka 1995, ili kukidhi matakwa na changamoto za udhibiti wa matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Baraza la Mawaziri liliagiza kuundwa kwa chombo cha kupambana na dawa za kulevya chenye uwezo kiutendaji kwa kukipa mamlaka ya ukamataji, upekuzi na upelelezi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuongeza ufanisi wa udhibiti wa dawa za kulevya nchini.
Kufuatia agizo hilo, tarehe 24/03/2015 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga na kupitisha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya Mwaka 2015 na kuanza kutumika rasmi tarehe 15 Septemba, 2015 kupitia tangazo la Serikali namba 407 (GN NO.407/2015).
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ilianza kutekeleza majukumu yake kikamilifu tarehe 17 Februari, 2017 baada Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Kamishna Jenerali.
Majukumu
Majukumu ya Mamlaka ni kufafanua, kuhamasisha, kuratibu na kutekeleza hatua zote zinazoelekezwa katika udhibiti wa dawa za kulevya. Katika kutekeleza majukumu hayo Mamlaka inafanya kazi zifuatazo:
i.Kusimamia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa, maazimio na makubaliano katika kudhibiti dawa za kulevya.
ii.Kuandaa na kutekeleza mpango wa Taifa wa kudhibiti dawa za kulevya.
iii.Kutengeneza miongozo inayoelezea tatizo la dawa za kulevya na madhara yake katika jamii;
iv.Kuboresha na kurekebisha sheria na kanuni za udhibiti wa dawa za kulevya;
v.Kuhamasisha udhibiti wa matumizi na biashara ya dawa za kulevya ikiwemo kutoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya, kusambaza taarifa kwa umma na juhudi nyingine za udhibiti;
vi.Kuchukua hatua stahiki za kupambana na biashara ya dawa za kulevya zikiwemo kukamata, kupekua na uchunguzi wa masuala yanayohusiana na dawa za kulevya.
vii.Kuzuia, kupeleleza na kuchunguza uchepushaji wa dawa za tiba zenye madhara ya kulevya pamoja na kemikali zilizosajiliwa kutoka kwenye vyanzo halali wakati huo huo kuhakikisha dawa hizo zinapatikana kwa matumizi ya tiba, biashara na mahitaji ya kisayansi;
viii.Kuanzisha mfumo thabiti wa ukusanyaji taarifa na uchambuzi katika ngazi ya taifa kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya;
ix.Kuhamasisha, kuratibu na kuhakikisha jitihada za ushirikiano wa kimataifa katika kudhibiti wa dawa za kulevya zinaimarishwa;
x.Kufanya, kuwezesha na kuratibu tafiti zinazohusiana na dawa za kulevya;
xi.Kuratibu na kuwezesha wadau wanaojihusisha na udhibiti wa matumizi na biashara ya dawa za kulevya;
xii.Kuelimisha na kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya;
xiii.Kutoa mafunzo kwa watendaji wanaojihusisha na udhibiti wa matumizi na biashara ya dawa za kulevya, fedha haramu na kemikali bashirifu.
xiv.Kufanya uchunguzi wa sayansi jinai.

Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)